Old/New Testament
7 Ndipo kuhani mkuu alimwuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?” 2 Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, ali pokuwa Mesopotamia, kabla hajahamia Harani, 3 akamwambia, ‘Ondoka kutoka katika nchi yako na kutoka kwa jamii yako uende katika nchi nitakayokuonyesha.’ 4 Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakal dayo akaenda kukaa Harani. Baba yake alipokufa, Mungu akamtoa huko akamweka katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. 5 Lakini Mungu hakumpa urithi wo wote katika nchi hii, hakumpa hata mita moja ya ardhi. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto. 6 Mungu alimwambia maneno haya, ‘Wazao wako wataishi ugenini, ambapo watafanywa kuwa watumwa na kutendewa maovu kwa kipindi cha miaka mia nne. 7 Lakini nitalihukumu taifa ambalo watalitumikia, na baada ya haya watatoka katika nchi hiyo ili waje kuniabudu mahali hapa.’
8 “Mungu akampa Ibrahimu agano la tohara. Basi Ibrahimu akawa baba wa Isaka; naye akamtahiri Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake. Isaka akawa baba wa Yakobo, naye Yakobo akawa baba wa babu zetu kumi na wawili. 9 Hawa babu zetu walimwonea Yusufu ndugu yao wivu, wakamwuza utumwani Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye. 10 Akamwokoa katika mateso yote yaliyom pata, na akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, Mfalme wa Misri, ambaye alimfanya waziri mkuu wa nchi nzima na mtawala wa nyumba ya mfalme.
11 “Kukawa na njaa na dhiki kubwa nchi yote ya Misri na Kanaani, na babu zetu wakawa hawana chakula. 12 Lakini Yakobo aliposikia kwamba kule Misri kulikuwa na nafaka, aliwatuma wanawe, wakaenda huko kwa mara yao ya kwanza. 13 Nao walipotumwa mara ya pili, Yusufu alijitambulisha kwa ndugu zake, na akawatam bulisha ndugu zake kwa Farao. 14 Yusufu akatuma Yakobo baba yake aletwe Misri pamoja na ukoo mzima, wakiwa ni watu sabini na watano; na 15 Yakobo akaenda Misri. Naye akafa huko, yeye na wanawe, yaani babu zetu, 16 na miili yao ikachukuliwa na kuzikwa huko Shekemu katika kaburi ambalo Ibrahimu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori. 17 Ulipokaribia wakati Mungu aliopanga kutimiza ahadi yake, kwa Ibrahimu, idadi ya watu iliongezeka sana huko Misri. 18 Ndipo akatokea mfalme mpya wa Misri ambaye hakumfahamu wala kumtambua Yusufu. 19 Huyu mfalme aliwafanyia hila watu wa taifa letu na akawalazimisha babu zetu wawatupe watoto wao wachanga ili wafe.
20 “Musa alizaliwa wakati huo, naye alikuwa mtoto mzuri sana machoni pa Mungu. Akalelewa na wazazi wake kwa muda wa miezi mitatu. 21 Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe.
Copyright © 1989 by Biblica