Old/New Testament
21 Alipokuwa Hekaluni Yesu aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la sadaka. 2 Akamwona na mama mmoja mjane, maskini sana, akiweka humo sarafu mbili. 3 Akasema, “Nawaambia kweli, huyu mjane ametoa sadaka kubwa zaidi kuliko hao wengine wote. 4 Kwa maana hao wengine wametoa sehemu ndogo tu ya utajiri wao, lakini yeye, ingawa ni maskini, ametoa vyote alivyokuwa navyo.”
Dalili Za Siku Za Mwisho
5 Baadhi ya watu walikuwa wakizungumza kuhusu Hekalu jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na mapambo maridadi yaliyotolewa kama sadaka kwa Mungu. Yesu akawaambia, 6 “Wakati unakuja ambapo vyote hivyo mnavyovistaajabia sasa vitabomolewa, halitabaki hata jiwe moja juu ya jingine.” 7 Wakamwuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kwamba yanakari bia?” 8 Akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja wakitumia jina langu, na kusema, ‘Mimi ndiye’ na ‘Wakati umekaribia’. Msiwafuate. 9 Na mtakaposikia habari za vita na machafuko, msiogope, kwa maana hayo ni lazima yatokee kwanza, ila mwisho hautatokea wakati huo.”
10 Kisha akawaambia: “Taifa moja litapigana na taifa lin gine na utawala mmoja utapigana na utawala mwingine. 11 Kutaku wepo na matetemeko ya ardhi, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali; kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.”
Mateso
12 “Lakini kabla haya yote hayajatokea watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Mtashtakiwa mbele ya wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani; na wengine mtapelekwa kushtakiwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu. 13 Na hii itawapa nafasi ya kutoa ushuhuda kuhusu imani yenu. 14 Lakini msiwe na wasiwasi juu ya matayarisho ya utetezi wenu kabla ya mashtaka. 15 Kwa maana nitawapa maneno na hekima ambayo maadui zenu hawa taweza kukataa au kupinga. 16 Mtasalitiwa na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu mtauawa. 17 Watu wote watawa chukia kwa ajili yangu. 18 Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu! 19 Simameni imara nanyi mtaokoa nafsi zenu.”
Copyright © 1989 by Biblica