Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Job for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 15:1-21

Wayahudi. 28 Wakakaa huko na wale wanafunzi kwa muda mrefu.

Baraza La Yerusalemu

15 Watu wengine walikuja Antiokia kutoka Yudea wakawa wakiwa fundisha ndugu walioamini kwamba, “Kama hamkutahiriwa kufuatana na desturi iliyofundishwa na Musa hamwezi kuokolewa.” Paulo na Barnaba walikuwa na mabishano makali nao wakipinga mafundisho haya. Ikaamuliwa kwamba Paulo na Barnaba na waamini wengine waende Yerusalemu wakawaulize mitume na wazee juu ya jambo hili. Kwa hiyo, wakiwa wametumwa na kanisa, njiani walipitia makanisa ya Foenike na Samaria wakatoa taarifa jinsi watu wa mataifa men gine walivyokuwa wakimgeukia Bwana. Habari hizi ziliwafurahisha sana hao ndugu. Walipofika Yerusalemu walipokelewa na kanisa, mitume na wazee; nao wakatoa taarifa kuhusu mambo yote ambayo Mungu aliyafanya kwa kuwatumia wao. Lakini baadhi ya waamini waliokuwa wakishikilia desturi za Mafarisayo wakasema, “Ni lazima watahiriwe na wafundishwe kushika sheria ya Musa.”

Mitume na wazee wa kanisa wakakutana kushauriana juu ya jambo hili. Baada ya majadiliano marefu, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za mwanzo Mungu alini chagua ili kwa midomo yangu watu wa mataifa mengine wapate kusi kia Habari Njema na kuamini. Na Mungu ambaye anajua mioyo ya watu alishuhudia kwamba anawakubali watu wa mataifa kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa na sisi. Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa sababu waliamini. 10 Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hawa ndugu wanafunzi mzigo wa sheria ambao baba zetu na sisi tumesh indwa kuubeba? 11 Sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Yesu, kama na wao wanavyookolewa.” 12 Baraza lote likakaa kimya; wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa mataifa. 13 Walipomaliza maelezo yao, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. 14 Simoni amekwisha kutueleza jinsi, kwa mara ya kwanza, Mungu amejichagulia waamini kutoka kwa watu wa mataifa. 15 Hata maneno ya manabii yanakubaliana kabisa na jambo hili. Kama ilivyoandikwa: 16 ‘ Baada ya mambo haya nitarudi, nami nitajenga upya nyumba ya Daudi ambayo imeanguka. Nitajenga tena magofu yake na kuisimamisha, 17 ili binadamu wengine wote wamtafute Bwana, pamoja na watu wa mataifa yote ambao wanaitwa kwa jina langu; 18 asema Bwana, ambaye ametufahamisha mambo hayo tangu kale.’

19 “Kwa hiyo uamuzi wangu ni kwamba, tusiwasumbue watu wa mataifa wanaomgeukia Mungu kwa desturi zetu; 20 badala yake, tuwaandikie barua tuwaambie wajiepushe na uchafu wa ibada za sanamu, na zinaa na waache kula nyama ya wanyama walionyongwa au kunywa damu. 21 Kwa maana sheria za Musa zimekuwa zikihubiriwa katika kila mji na kusomwa katika masinagogi kila sabato tangu vizazi vya awali.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica