Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: 2Sam for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Wagalatia 1

Salamu kutoka kwa mtume Paulo. Sikutumwa na kundi lolote la watu au mtu yeyote hapa duniani niwe mtume. Sikupewa mamlaka yangu na mwanadamu yeyote. Nilipewa mamlaka haya moja kwa moja kutoka kwa Kristo Yesu[a] na Mungu Baba, aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu. Salamu pia kutoka kwa wote walio familia ya Mungu, walio pamoja nami.

Kwa makanisa yaliyoko Galatia:[b]

Namwomba Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo awe mwema kwenu na awape neema na amani. Yesu alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili atuweke huru kutoka katika uovu wa ulimwengu huu tunamoishi. Hili ndilo Mungu Baba yetu alitaka. Mungu Baba yetu anastahili utukufu milele na milele! Amina.

Kuna Ujumbe Mmoja tu wa Habari Njema

Wakati mfupi tu uliopita Mungu aliwaita mkamfuata. Aliwaita katika neema yake kwa njia ya Kristo. Lakini sasa nashangazwa kwamba kwa haraka hivi mmegeuka mbali na kuamini kitu kingine tofauti kabisa na Habari Njema tuliyowahubiri. Hakuna ujumbe mwingine wa Habari Njema, lakini baadhi ya watu wanawasumbua. Wanataka kuibadili Habari Njema ya Kristo. Tuliwahubiri ninyi ujumbe wa Habari Njema tu. Hivyo laana ya Mungu impate mtu yeyote yule anayewahubiri ninyi ujumbe ulio tofauti, hata ikiwa ni mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni! Nitalisema tena lile nililolisema hapo mwanzo. Ninyi mmekwishaipokea Habari Njema. Yeyote atakayewahubiri kitu kingine tofauti na ile Habari Njema mliyoipokea, basi mjue kwamba Mungu atamlaani mtu huyo!

10 Sasa mnafikiri ninajaribu kuwapendeza wanadamu? Hapana, ninataka kumpendeza Mungu siyo wanadamu. Kama ningekuwa najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumwa wa Kristo.

Mamlaka ya Paulo ni Kutoka kwa Mungu

11 Ndugu zangu, ninawataka mjue kuwa ujumbe wa Habari Njema niliowaambia haukuandaliwa na mtu yeyote. 12 Sikuupata ujumbe wangu kutoka kwa mwanadamu yeyote. Habari Njema siyo kitu nilichojifunza kutoka kwa watu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia Habari Njema ninayowahubiri watu.

13 Mmesikia juu ya mwenendo wangu hapo zamani nilipokuwa mfuasi hodari wa dini ya Kiyahudi. Nililitesa kwa nguvu kanisa la Mungu, nikiwa na shabaha ya kuliangamiza kabisa. 14 Nilipata maendeleo makubwa katika dini ya Kiyahudi kwa kufanya kazi na kusoma kwa bidii kwa sababu nilikuwa mwaminifu kwa desturi za baba zetu.

15 Lakini Mungu alikuwa na mpango maalumu kwa ajili yangu hata kabla sijazaliwa.[c] Hivyo aliniita kwa neema yake. Na ilimpendeza 16 kumfunua Mwanaye ili niweze kuwahubiri Habari Njema watu wasio Wayahudi. Hicho ndicho nilichofanya baada ya hapo. Sikuomba ushauri ama msaada wowote kutoka kwa mtu yeyote. 17 Sikwenda Yerusalemu kuwaona wale waliokuwa mitume kabla mimi sijawa mtume. Badala yake, kwanza nilienda moja kwa moja Arabia. Kisha baadaye, nikarudi katika mji wa Dameski.

18 Miaka mitatu baadaye nilikwenda Yerusalemu kumwona Petro.[d] Nilikaa naye kwa siku 15. 19 Sikuonana na mtume mwingine yeyote, isipokuwa Yakobo mdogo wake Bwana peke yake. 20 Mungu anajua kuwa hakuna ninachowaandikia kisicho cha kweli. 21 Baadaye, nilielekea katika majimbo ya Shamu na Kilikia.

22 Lakini kwa wakati ule, makanisa ya Kristo yaliyokuwa Uyahudi yalikuwa bado hayajanifahamu mimi binafsi. 23 Walikuwa wamesikia tu juu yangu: “Mtu huyu alikuwa anatutesa. Lakini sasa anawaambia watu juu ya imani ile ile aliyojaribu kuiangamiza huko nyuma.” 24 Waamini hawa walimsifu Mungu kwa sababu yangu.

Error: Book name not found: Ezek for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International