Print Page Options Listen to John 19-21
Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Yohana 19-21

Yesu Ahukumiwa Kifo

19 Ndipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe viboko. Askari wakasuka taji ya miiba wakamwekea Yesu kichwani, wakamvika na kanzu ya zambarau.

Lakini walipomkaribia Yesu wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu.

Mfalme wa Wayahudi!’

Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na kanzu ya zambarau. Pilato akawaambia, “Huyu hapa mtu wenu.” Wale makuhani wakuu na viongozi wa Wayahudi walipomwona wakapiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawajibu, “Mchukueni mumsulubishe ninyi, kwa sababu mimi sioni kosa alilo tenda.” Wao wakamjibu, “Sisi tunayo sheria ambayo inamhukumu kifo kwa sababu yeye anajiita Mwana wa Mungu.” Pilato aliposi kia haya aliingiwa na hofu. Akaingia ukumbini tena akamwuliza Yesu, “Wewe unatoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. 10 Pilato akamwambia, “Kwa nini hunijibu? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachilia huru au kukusulubisha?” 11 Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka ye yote juu yangu kama Mungu hakukupa mamlaka hayo; kwa hiyo mtu aliyenishtaki kwako ana dhambi kubwa zaidi.” 12 Tangu wakati huo Pilato akaanza kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakasema, “Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayejifanya kuwa mfalme anampinga Kaisari.” 13 Pilato aliposi kia maneno haya alimtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha kuhukumia, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe - kwa Kiebrania paliitwa Gabatha.

14 Siku hiyo ilikuwa ni siku moja kabla ya Pasaka, siku iliyoitwa siku ya Matayarisho, yapata kama saa sita hivi. Pilato Akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa Mfalme wenu!” 15 Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe Mfalme wenu?” Wale makuhani wakuu wakamjibu, “Hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.” 16 Ndipo Pilato akawaka bidhi Yesu wamsulubishe.

Yesu Asulubishwa

17 Kwa hiyo wakamchukua Yesu, naye akatoka akiwa amebeba msalaba wake kuelekea mahali palipoitwa, ‘Fuvu la kichwa,’ au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubishwa watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia wa Yesu. 19 Pilato aliandika maneno yafuatayo kwenye kibao, kikawekwa juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI” 20 Kwa kuwa mahali hapo palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maneno haya ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kilatini na Kigiriki. 21 Makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali ‘Mtu huyu alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.”’ 22 Pilato akawajibu, “ Nilichokwisha andika, nimeandika.”

Mavazi Ya Yesu Yagawanywa

23 Maaskari walipokwisha msulubisha Yesu, walichukua mavazi yake wakayagawa mafungu manne; kila askari akapata moja. Ila wal ikubaliana wasipasue ile kanzu yake kwa maana ilikuwa imefumwa tangu juu hadi chini na haikukatwa mahali po pote. 24 Wakaam biana, “Tusiipasue ila tupige kura tuone ni nani aichukue.” Hii ilitimiza yale Maandiko yaliyosema, “Waligawana mavazi yangu, na kanzu yangu wakaipigia kura.” 25 Kwa hiyo wakapiga kura. Karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Mariamu mama yake, shan gazi yake, Mariamu mke wa Klopa na Mariamu Magdalena. 26 Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, huyo ni mwanao!” 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Na huyo ni mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.

Kifo Cha Yesu

28 Baada ya haya Yesu alifahamu ya kuwa mambo yote yameka milika, kwa hiyo, ili kutimiza Maandiko, akasema, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo wakampandishia mdomoni. 30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.

31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani. 32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji. 35 Mambo haya yamehakikishwa na mtu aliyeyaona, na ushahidi wake ni wa kuaminika. Yeye anajua ya kuwa aliyosema ni kweli, naye ametoa ushuhuda huu ili nanyi mpate kuamini. 36 Kwa maana mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Na pia Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.” 38 Baada ya haya, Yusufu wa Arimathea aliyekuwa mfuasi wa siri wa Yesu, maana aliwaogopa Wayahudi, akamwomba Pilato auchukue mwili wa Yesu; naye akamruhusu. Kwa hiyo akaja, akauchukua mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye alimwen dea Yesu kwa siri usiku, alikuja na mchanganyiko wa manukato zaidi ya kilo thelathini. 40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakau vika sanda iliyokuwa na manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Way ahudi. 41 Karibu na pale walipomsulubisha palikuwa na bustani yenye kaburi ambalo lilikuwa halijatumika. 42 Kwa hiyo ili kuka milisha mazishi kabla ya sabato, wakamzika Yesu kwenye hilo kab uri lililokuwa karibu.

Kaburi Tupu

20 Jumapili asubuhi na mapema, kukiwa bado giza, Mariamu Mag dalena alifika kaburini akakuta lile jiwe lililokuwa limeziba mlango wa kaburi limeondolewa. Kwa hiyo akaenda mbio kwa Simoni Petro na yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akawaambia, “Wameu chukua mwili wa Bwana kutoka mle kaburini na hatujui wameuweka wapi!” Petro na yule mwanafunzi wakaondoka mara kuelekea kabu rini. Wote wawili walikuwa wanakimbia lakini yule mwanafunzi akakimbia mbio zaidi kuliko Petro, akawahi kufika kaburini. Alipofika akainama na kuchungulia mle kaburini akaona ile sanda, lakini hakuingia ndani. Ndipo Petro akaja akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani ya kaburi. Naye akaona ile sanda na kile kitambaa kilichokuwa kichwani mwa Yesu kimekunjwa na kuwekwa kando ya ile sanda. Kisha yule mwanafunzi aliyewahi kufika kaburini naye akaingia ndani; akaona, akaamini. Kwa maana mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa yale Maandiko yaliyotabiri kuwa angefufuka kutoka kwa wafu. 10 Wale wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.

Yesu Anamtokea Mariamu

11 Lakini Mariamu akakaa nje ya kaburi akilia. Na alipokuwa akilia akainama kutazama mle kaburini. 12 Akaona malaika wawili wamevaa nguo nyeupe, wamekaa pale mwili wa Yesu ulipokuwa, mmoja upande wa miguuni na mwingine upande wa kichwani! 13 Wakamwuliza Mariamu, “Mama, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui wamemweka wapi.” 14 Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita, “Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania, “Rabboni!’ 17 Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”

Yesu Anawatokea Wanafunzi Wake

19 Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi sana walipomwona Bwana! 21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.” 22 Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake, atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”

Yesu Anamtokea Tomaso

24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”

26 Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa, lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani iwe nanyi.” 27 Ndipo akamwambia Tomaso, “Weka kidole chako hapa; tazama mikono yangu halafu nyoosha mkono wako uguse ubavu wangu. Usiwe na mashaka bali uamini.” 28 Tomaso akasema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” 29 Yesu akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”

30 Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele za wanafunzi wake ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Yesu Ajitambulisha Kwa Wanafunzi Saba

21 Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.” Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.

Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.” 11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.

Yesu Amwuliza Petro Kama Anampenda

15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate.” 20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’ 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”

24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake ni wa kweli.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica