Book of Common Prayer
23 Ninawaambia hili, na ninamwomba Mungu awe shahidi wangu kuwa ni la kweli: Sababu iliyonifanya nisirudi tena Korintho ni kuwa nilitaka niepuke kuwapa karipio lenye nguvu. 24 Sina maana ya kuwa tunataka kuitawala imani yenu. Ninyi mpo imara katika imani. Lakini tunatenda kazi pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu wenyewe.
2 Hivyo niliamua moyoni mwangu mwenyewe kuwa sitafanya safari nyingine ya huzuni kuja kwenu. 2 Ikiwa nitawafanya muwe na huzuni nani atanifanya niwe na furaha? Ni ninyi tu ndiyo mnaweza kunifanya niwe na furaha. Ni ninyi ambao niliwahuzunisha. 3 Naliwaandikia barua ili kwamba nijapo kwenu nisihuzunishwe na wale ambao wanapaswa kunifanya niwe na furaha. Nilijisikia kuwa na hakika ya kuwa ninyi nyote mtashiriki furaha yangu. 4 Nilipowaandikia barua ya kwanza, niliiandika macho yangu yakibubujika machozi mengi. Sikuandika ili kuwafanya muwe na huzuni, bali kuwafanya mjue kwa jinsi gani ninavyowapenda.
Msamehe Mtu Aliye Fanya Kosa
5 Mtu mmoja katika kusanyiko lenu amesababisha maumivu, ila si kwangu, bali amesababisha maumivu kwenu nyote kwa kiwango fulani. Nina maanisha amewakwaza nyote kwa namna fulani. (Sitaki ionekane kuwa mbaya sana kuliko ilivyo) 6 Adhabu ambayo walio wengi miongoni mwa kusanyiko lenu walimpa inatosha. 7 Lakini msameheni na kumtia moyo sasa. Hili litamsaidia asiwe na huzuni sana na asikate tamaa kabisa. 8 Hivyo ninawasihi mwonesheni kuwa mnampenda. 9 Hii ndiyo sababu niliandika ile barua. Nilitaka kuwapima na kuona ikiwa mna utii katika kila kitu. 10 Mkimsamehe mtu, ndipo nami husamehe pia. Na kile nilichosamehe, kama nilikuwa na jambo la kusamehe, nilisamehe kwa ajili yenu. Na Kristo akithibitisha. 11 Nilifanya hivi ili Shetani asipate ushindi wowote kutoka kwetu. Tunafahamu sote mipango yake ilivyo.
Yesu Atoa Simulizi Kuhusu Shamba la Mzabibu
(Mt 21:33-46; Lk 20:9-19)
12 Yesu alianza kuongea nao kwa simulizi zenye mafumbo: “Mtu mmoja alipanda mizabibu shambani. Akajenga ukuta kuizunguka, akachimba shimo kwa ajili ya kukamulia mizabibu na kisha alijenga mnara. Baadaye alilikodisha kwa baadhi ya wakulima na akaenda safari nchi ya mbali.
2 Yalipotimia majira ya kuvuna, alimtuma mtumishi wake kwa wakulima wale, ili kukusanya sehemu yake ya matunda ya mzabibu. 3 Lakini wakulima wale walimkamata mtumishi yule, wakampiga, na kumfukuza pasipo kumpa chochote. 4 Kisha akamtuma mtumishi mwingine kwao. Huyu naye wakampiga kichwani na kumtendea mambo ya aibu. 5 Yule mmiliki wa shamba la mzabibu akamtuma mtumishi mwingine, na wakulima wale wakamuua na yule pia. Baada ya hapo alituma wengi wengine. Wakulima wale waliwapiga baadhi yao na kuua wengine.
6 Hata hivyo mwenye shamba yule bado alikuwa na mmoja wa kumtuma, mwanaye mpendwa. Alimtuma akiwa mtu wa mwisho. Akasema, ‘nina hakika watamheshimu mwanangu!’
7 Lakini wakulima wale walisemezana wao kwa wao, ‘Huyu ndiye yule mrithi. Njooni tukamuue, na urithi utakuwa wetu!’ 8 Kwa hiyo wakamchukua na kumuua, kisha wakautupa mwili wake nje ya shamba la mizabibu.
9 Je! Mnadhani mwenye kumiliki lile shamba la mizabibu atafanya nini? Atakuja na kuwaua wakulima wale, na kukodisha shamba lile kwa watu wengine. 10 Je! Hamjayasoma maandiko haya:
‘Jiwe ambalo wajenzi wamelikataa
limekuwa jiwe kuu la msingi.
11 Hii imefanywa na Bwana
na ni ajabu kubwa kwetu kuona!’”(A)
© 2017 Bible League International