Marko 14
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mpango wa Kumwua Yesu
(Mt 26:1-5; Lk 22:1-2; Yh 11:45-53)
14 Ilikuwa yapata siku mbili kabla ya Sikukuu ya Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Wakuu wa makuhani na walimu wa Sheria walikuwa wakitafuta njia, kwa ujanja fulani, ya kumkamata na kumuua Yesu. 2 Kwani walikuwa wakisema “tusifanye hivi wakati wa sherehe, ama sivyo watu watafanya fujo.”
Mwanamke Ampa Yesu Heshima
(Mt 26:6-13; Yh 12:1-8)
3 Yesu alikuwa Bethania, katika nyumba ya Simoni mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi. Wakati ameketi mezani mwanamke mmoja alimwijia. Naye alikuwa na gudulia la mawe lililojaa manukato ya bei ghali yaliyotengenezwa kwa nardo safi. Mwanamke huyo alilifungua gudulia lile kwa kulivunja na kumwagia Yesu manukato kichwani mwake.
4 Baadhi ya watu waliokuwa pale walikasirika na kulalamika miongoni mwao, “Kwa nini kuwepo na ufujaji wa manukato namna hii? 5 Gharama yake ni sawa na mshahara wa mwaka[a] mzima. Manukato haya yangeweza kuuzwa na fedha hiyo kupewa walio maskini.” Kisha wakamkosoa yule mwanamke kwa hasira kwa jambo alilolifanya.
6 “Lakini Yesu alisema mwacheni peke yake. Kwa nini mnamsumbua? Yeye amenifanyia kitendo chema. 7 Kwani siku zote mnao maskini pamoja nanyi na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaopenda. Lakini hamtakuwa pamoja nami siku zote. 8 Yeye amefanya kile alichokiweza kufanya. Ameumwagia manukato mwili wangu kabla ya wakati kuuandaa kwa ajili ya maziko. 9 Ninawaambia kweli: Popote injili itakapohubiriwa ulimwenguni, kile alichokifanya kitasimuliwa kwa kumkumbuka.”
Yuda Akubali Kuwasaidia Adui wa Yesu
(Mt 26:14-16; Lk 22:3-6)
10 Kisha Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na mbili, aliwaendea viongozi wa makuhani ili kumsaliti Yesu kwao. 11 Nao walifurahi kusikia hivyo, na wakaahidi kumpa fedha. Kwa hiyo Yuda akaanza kutafuta wakati unaofaa wa kumsaliti.
Karamu ya Pasaka
(Mt 26:17-25; Lk 22:7-14,21-23; Yh 13:21-30)
12 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, ambapo kila mara mwana kondoo alitolewa sadaka kwa ajili ya Pasaka. Wanafunzi wa Yesu wakamwendea na kumwuliza, “Ni wapi unapotaka tuende kukuandalia ili uweze kuila Karamu ya Pasaka?”
13 Hivyo Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili, naye akawaeleza, “ingieni mjini, na mtakutana na mtu mmoja aliyebeba gudulia la maji. Mfuateni, 14 popote pale atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba ile, ‘mwalimu anasema, utuonyeshe chumba ambacho yeye na wanafunzi wake wanaweza kuila Karamu ya Pasaka.’ 15 Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, klichoandaliwa tayari kwa ajili yetu. Basi mtuandalie chakula pale.”
16 Wanafunzi wa Yesu waliondoka na kuelekea mjini. Huko walikuta kila kitu kama vile Yesu alivyowaeleza Hivyo, waliandaa mlo wa Pasaka.
17 Wakati wa jioni Yesu alienda pamoja na wanafunzi wake kumi na mbili katika nyumba ile. 18 Wote walipokuwa wameketi mezani wakila, Yesu akasema, “Mniamini ninapowambia kwamba mmoja wenu, yule anayekula nami sasa atanitoa kwa maadui zangu.”
19 Wanafunzi walihuzunika sana kusikia jambo hili. Kila mmoja akamwambia Yesu, “Hakika siyo mimi?”
20 Akawaambia, “Ni mmoja wa wale kumi na mbili; na ni yule atakayechovya mkate katika bakuli pamoja nami. 21 Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama ilivyoandikwa juu yake. Lakini itakuwa ya kutisha namna gani kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu anasalitiwa. Itakuwa bora mtu huyu asingelikuwa amezaliwa.”
Chakula cha Bwana
(Mt 26:26-30; Lk 22:15-20; 1 Kor 11:23-25)
22 Na walipokuwa wakila Yesu aliuchukua mkate, akamshukuru Mungu kwa huo. Akamega vipande, akawapa wanafunzi wake, na kusema, “Chukueni na mle mkate huu. Ni mwili wangu.”
23 Kisha akakichukua kikombe chenye divai, akamshukuru Mungu kwa hicho, akawapa. Wote wakanywa toka kile kikombe. 24 Kisha akasema, “Kinywaji hiki ni damu yangu ambayo kwayo Mungu anafanya agano na watu wake. Damu yangu inamwagika kwa manufaa ya watu wengi. 25 Ninawaambia kweli sitakunywa diva tena mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya katika Ufalme wa Mungu.”
26 Na wao wakaimba mwimbo wa sifa na kutoka na kuelekea kwenye Mlima wa Miti ya Mizeituni.
Yesu Asema Wafuasi Wake Watamwacha
(Mt 26:31-35; Lk 22:31-34; Yh 13:36-38)
27 Yesu akawaambia, “Nyote mtaniacha, kwani imeandikwa,
‘Nitamuua mchungaji,
na kondoo watatawanyika.’(A)
28 Lakini baada ya kuuawa, nitafufuka kutoka kwa wafu. Kisha nitaenda Galilaya. Nitakuwa pale kabla ninyi hamjafika.”
29 Lakini Petro akamwambia, “Hata kama wengine wote watapoteza imani yao, mimi sitapoteza imani yangu.”
30 Ndipo Yesu akamjibu kusema, “Ukweli ni kwamba, usiku wa leo utasema kuwa hunijui. Utasema hivyo mara tatu kabla ya jogoo kuwika mara mbili.”
31 Petro akasema kwa kusisitiza zaidi, “Hata kama itanipasa kufa nawe, sitasema kuwa sikujui.” Na wengine wakasema hivyo.
Yesu Aomba Akiwa Peke Yake
(Mt 26:36-46; Lk 22:39-46)
32 Kisha wakafika mahali palipoitwa Gethsemane. Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati ninaomba.” 33 Naye Yesu akamchukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye, naye akaanza kusumbuka sana. 34 Akawaambia, “Nina huzuni sana na ninafikiri inaweza kuniua. Kaeni hapa, na mjihadhari.”
35 Akiendelea mbele kidogo, alianguka chini, na akaomba ikiwezekana angeiepuka saa ya mateso. 36 Akasema, “Aba,[b] yaani Baba, vyote vinawezekana kwako wewe. Hebu kiondoe kikombe[c] hiki kutoka kwangu, Lakini usifanye kama ninavyopenda mimi, lakini kama unavyopenda wewe.”
37 Kisha Yesu akaja na kuwakuta wamelala, na akamwuliza Petro, “Simoni, je umelala? Je, hukuweza kukaa macho kwa muda wa saa moja tu? 38 Kaeni macho na kuomba, ili msije mkaingia majaribuni. Roho inataka lakini mwili ni dhaifu.”
39 Yesu akaondoka kwenda kuomba tena, akilisema jambo lile lile. 40 Kisha akarudi tena na kuwakuta wamelala, kwani macho yao yalikuwa yamechoka. Wao hawakujua la kusema kwake.
41 Alirudi mara ya tatu na kuwaambia, “Je, bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imefika. Mwana wa Adamu atasalitiwa mikononi mwa watenda dhambi. 42 Amkeni! Twendeni! Tazama! Yule atakayenisaliti amekaribia.”
Yesu Akamatwa
(Mt 26:47-56; Lk 22:47-53; Yh 18:3-12)
43 Mara moja, wakati Yesu akali akizungumza, Yuda, mmoja wa wale kumi na mbili, alitokea. Pamoja naye walikuwa kundi kubwa la watu waliokuwa na majambia na marungu wakitoka kwa viongozi wa makuhani, walimu wa sheria na wazee.
44 Msaliti alikuwa tayari amewapa ishara: “Yule ambaye nitambusu ndiye mwenyewe. Mkamateni, mlindeni na muwe waangalifu mnapomwondoa.” 45 Mara tu Yuda alipowasili, alimwendea Yesu. Alipomkaribia alisema, “Mwalimu!” Kisha akambusu. 46 Ndipo walipomkamata na kumshikilia. 47 Mmoja wa wale waliosimama naye karibu akautoa upanga wake alani, akampiga nao mtumishi wa kuhani mkuu na kulikata sikio lake.
48 Kisha Yesu akawaambia, “Je, mlikuja kunikamata kwa upanga na marungu, kama vile mimi nimekuwa jambazi? 49 Kila siku nilikuwa nanyi, nikifundisha Hekaluni na hamkujaribu kunikamata wakati huo. Lakini Maandiko lazima yatimie.” 50 Wafuasi wake wote walimwacha na kumkimbia.
51 Miongoni mwa watu waliomfuata Yesu alikuwa kijana mmoja aliyevaa kipande cha nguo. Watu walipotaka kumkamata 52 alikiacha kile kipande cha nguo mikononi mwao na kukimbia akiwa uchi.
Yesu Akiwa Mbele ya Viongozi wa Kidini
(Mt 26:57-68; Lk 22:54-55,63-71; Yh 18:13-14,19-24)
53 Nao wakamwongoza Yesu kumpeleka kwa kuhani mkuu, na viongozi wote wa makuhani, wazee, na walimu wa Sheria walikutanika. 54 Petro akamfuata Yesu kwa mbali kidogo hadi ndani ya baraza la nyumba ya kuhani mkuu. Petro alikuwa ameketi na wale walinzi akijipasha joto na moto walioukoka.
55 Viongozi wa makuhani na Baraza lote la Wayahudi walikuwa wakitafuta ushahidi dhidi ya Yesu wa kuweza kumhukumu kifo, lakini hawakupata kitu chochote. 56 Watu wengi walikuja na kutoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini wote walisema vitu tofauti. Ushahidi wao ulipingana.
57 Kisha wengine walisimama na kushuhudia kinyume chake kwa uongo, wakisema, 58 “Tulimsikia mtu huyu[d] akisema, ‘Nitaliharibu Hekalu hili lililotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, na kwa siku tatu nitajenga lingine ambalo halikujengwa kwa mikono.’” 59 Lakini hata katika ushahidi wao huu hawakukubaliana.
60 Kisha kuhani mkuu akasimama mbele yao na akamwuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Nini ushahidi huu ambao watu wanaleta dhidi yako?” 61 Lakini Yesu alinyamaza kimya na hakutoa jibu lolote.
Kwa mara nyingine kuhani mkuu akamwuliza, “Je, wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu anayesifiwa?”
62 Yesu akasema, “Mimi ndiye. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye uweza wote akija pamoja na mawingu ya mbinguni.”[e]
63 Kuhani mkuu alichana mavazi yake na kusema, “Tuna haja gani ya kuleta mashahidi zaidi? 64 Ninyi wote mmesikia akimtolea Mungu matusi.”
Wote walimhukumu na kumwona kwa anastahili kifo. 65 Na wengine walianza kutema mate, na kufunika uso wake, na kumpiga, na kumwambia, “Uwe nabii na utuambie nani aliyekupiga.” Kisha wale walinzi walimchukua na kuendelea kumpiga.
Petro Amkana Yesu
(Mt 26:69-75; Lk 22:56-62; Yh 18:15-18,25-27)
66 Wakati Petro alipokuwa bado barazani, mtumishi wa kike wa kuhani mkuu alifika pale. 67 Alipomwona Petro akijipasha moto, alimkazia macho na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu, Mnazareti.”
68 Lakini Petro alisema, “Hii si kweli, mie sifahamu wala kuelewa kile unachokisema.” Baada ya hapo Petro alitoka na kwenda barazani na hapo hapo jogoo akawika.
69 Yule mtumishi wa kike alipomwona alirudia tena kuwaeleza wale waliokuwa wamesimama pale, “Mtu huyu ni mmoja wao!” 70 Kwa mara nyingine tena Petro alikataa.
Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesimama pale wakarudia tena kumwambia Petro, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa sababu wewe pia ni Mgalilaya.”
71 Petro akaanza kutoa maneno makali na kusema, “Naapa kwa Mungu, simjui mtu huyu mnayemzungumzia!”
72 Mara jogoo akawika kwa mara ya pili, na Petro akakumbuka lile neno la Yesu alilomwambia: “Kabla kogoo hajawika mara ya pili utanikana mara tatu.” Naye akavunjika moyo na kuanza kulia.
Footnotes
- 14:5 mshahara wa mwaka Wa mwaka wa mtu kwa hali halisi “dinari 300” (sarafu za fedha). Sarafu moja, dinari ya Kirumi, ilikuwa ni wastani wa mshahara wa mtu wa siku moja.
- 14:36 Aba Ni neno la Kiaramu lililotumiwa na watoto wa Kiyahudi kama jina la kuwaita baba zao.
- 14:36 kikombe Kikombe ni ishara ya mateso. Yesu alitumia dhana ya kukinywea kikombe akimaanisha kuyakubali mateso ambayo angeyapata katika matukio ya kutisha ambayo yangetokea muda mfupi ujao.
- 14:58 mtu huyu Yaani, Yesu. Adui zake walikuwa wanakwepa kutamka jina lake.
- 14:62 Mwana wa Adamu … ya mbinguni Tazama Dan 7:13 na Zab 110:1.
Mark 14
New Century Version
The Plan to Kill Jesus
14 It was now only two days before the Passover and the Feast of Unleavened Bread. The leading priests and teachers of the law were trying to find a trick to arrest Jesus and kill him. 2 But they said, “We must not do it during the feast, because the people might cause a riot.”
A Woman with Perfume for Jesus
3 Jesus was in Bethany at the house of Simon, who had a skin disease. While Jesus was eating there, a woman approached him with an alabaster jar filled with very expensive perfume, made of pure nard. She opened the jar and poured the perfume on Jesus’ head.
4 Some who were there became upset and said to each other, “Why waste that perfume? 5 It was worth a full year’s work. It could have been sold and the money given to the poor.” And they got very angry with the woman.
6 Jesus said, “Leave her alone. Why are you troubling her? She did an excellent thing for me. 7 You will always have the poor with you, and you can help them anytime you want. But you will not always have me. 8 This woman did the only thing she could do for me; she poured perfume on my body to prepare me for burial. 9 I tell you the truth, wherever the Good News is preached in all the world, what this woman has done will be told, and people will remember her.”
Judas Becomes an Enemy of Jesus
10 One of the twelve apostles, Judas Iscariot, went to talk to the leading priests to offer to hand Jesus over to them. 11 These priests were pleased about this and promised to pay Judas money. So he watched for the best time to turn Jesus in.
Jesus Eats the Passover Meal
12 It was now the first day of the Feast of Unleavened Bread when the Passover lamb was sacrificed. Jesus’ followers said to him, “Where do you want us to go and prepare for you to eat the Passover meal?”
13 Jesus sent two of his followers and said to them, “Go into the city and a man carrying a jar of water will meet you. Follow him. 14 When he goes into a house, tell the owner of the house, ‘The Teacher says: “Where is my guest room in which I can eat the Passover meal with my followers?”’ 15 The owner will show you a large room upstairs that is furnished and ready. Prepare the food for us there.”
16 So the followers left and went into the city. Everything happened as Jesus had said, so they prepared the Passover meal.
17 In the evening, Jesus went to that house with the twelve. 18 While they were all eating, Jesus said, “I tell you the truth, one of you will turn against me—one of you eating with me now.”
19 The followers were very sad to hear this. Each one began to say to Jesus, “I am not the one, am I?”
20 Jesus answered, “It is one of the twelve—the one who dips his bread into the bowl with me. 21 The Son of Man will die, just as the Scriptures say. But how terrible it will be for the person who hands the Son of Man over to be killed. It would be better for him if he had never been born.”
The Lord’s Supper
22 While they were eating, Jesus took some bread and thanked God for it and broke it. Then he gave it to his followers and said, “Take it; this is my body.”
23 Then Jesus took a cup and thanked God for it and gave it to the followers, and they all drank from the cup.
24 Then Jesus said, “This is my blood which is the new[a] agreement that God makes with his people. This blood is poured out for many. 25 I tell you the truth, I will not drink of this fruit of the vine[b] again until that day when I drink it new in the kingdom of God.”
26 After singing a hymn, they went out to the Mount of Olives.
Jesus’ Followers Will Leave Him
27 Then Jesus told the followers, “You will all stumble in your faith, because it is written in the Scriptures:
‘I will kill the shepherd,
and the sheep will scatter.’ Zechariah 13:7
28 But after I rise from the dead, I will go ahead of you into Galilee.”
29 Peter said, “Everyone else may stumble in their faith, but I will not.”
30 Jesus answered, “I tell you the truth, tonight before the rooster crows twice you will say three times you don’t know me.”
31 But Peter insisted, “I will never say that I don’t know you! I will even die with you!” And all the other followers said the same thing.
Jesus Prays Alone
32 Jesus and his followers went to a place called Gethsemane. He said to them, “Sit here while I pray.” 33 Jesus took Peter, James, and John with him, and he began to be very sad and troubled. 34 He said to them, “My heart is full of sorrow, to the point of death. Stay here and watch.”
35 After walking a little farther away from them, Jesus fell to the ground and prayed that, if possible, he would not have this time of suffering. 36 He prayed, “Abba,[c] Father! You can do all things. Take away this cup[d] of suffering. But do what you want, not what I want.”
37 Then Jesus went back to his followers and found them asleep. He said to Peter, “Simon, are you sleeping? Couldn’t you stay awake with me for one hour? 38 Stay awake and pray for strength against temptation. The spirit wants to do what is right, but the body is weak.”
39 Again Jesus went away and prayed the same thing. 40 Then he went back to his followers, and again he found them asleep, because their eyes were very heavy. And they did not know what to say to him.
41 After Jesus prayed a third time, he went back to his followers and said to them, “Are you still sleeping and resting? That’s enough. The time has come for the Son of Man to be handed over to sinful people. 42 Get up, we must go. Look, here comes the man who has turned against me.”
Jesus Is Arrested
43 At once, while Jesus was still speaking, Judas, one of the twelve apostles, came up. With him were many people carrying swords and clubs who had been sent from the leading priests, the teachers of the law, and the Jewish elders.
44 Judas had planned a signal for them, saying, “The man I kiss is Jesus. Arrest him and guard him while you lead him away.” 45 So Judas went straight to Jesus and said, “Teacher!” and kissed him. 46 Then the people grabbed Jesus and arrested him. 47 One of his followers standing nearby pulled out his sword and struck the servant of the high priest and cut off his ear.
48 Then Jesus said, “You came to get me with swords and clubs as if I were a criminal. 49 Every day I was with you teaching in the Temple, and you did not arrest me there. But all these things have happened to make the Scriptures come true.” 50 Then all of Jesus’ followers left him and ran away.
51 A young man, wearing only a linen cloth, was following Jesus, and the people also grabbed him. 52 But the cloth he was wearing came off, and he ran away naked.
Jesus Before the Leaders
53 The people who arrested Jesus led him to the house of the high priest, where all the leading priests, the elders, and the teachers of the law were gathered. 54 Peter followed far behind and entered the courtyard of the high priest’s house. There he sat with the guards, warming himself by the fire.
55 The leading priests and the whole Jewish council tried to find something that Jesus had done wrong so they could kill him. But the council could find no proof of anything. 56 Many people came and told false things about him, but all said different things—none of them agreed.
57 Then some people stood up and lied about Jesus, saying, 58 “We heard this man say, ‘I will destroy this Temple that people made. And three days later, I will build another Temple not made by people.’” 59 But even the things these people said did not agree.
60 Then the high priest stood before them and asked Jesus, “Aren’t you going to answer? Don’t you have something to say about their charges against you?” 61 But Jesus said nothing; he did not answer.
The high priest asked Jesus another question: “Are you the Christ, the Son of the blessed God?”
62 Jesus answered, “I am. And in the future you will see the Son of Man sitting at the right hand of God, the Powerful One, and coming on clouds in the sky.”
63 When the high priest heard this, he tore his clothes and said, “We don’t need any more witnesses! 64 You all heard him say these things against God. What do you think?”
They all said that Jesus was guilty and should die. 65 Some of the people there began to spit at Jesus. They blindfolded him and beat him with their fists and said, “Prove you are a prophet!” Then the guards led Jesus away and beat him.
Peter Says He Doesn’t Know Jesus
66 While Peter was in the courtyard, a servant girl of the high priest came there. 67 She saw Peter warming himself at the fire and looked closely at him.
Then she said, “You also were with Jesus, that man from Nazareth.”
68 But Peter said that he was never with Jesus. He said, “I don’t know or understand what you are talking about.” Then Peter left and went toward the entrance of the courtyard. And the rooster crowed.[e]
69 The servant girl saw Peter there, and again she said to the people who were standing nearby, “This man is one of those who followed Jesus.” 70 Again Peter said that it was not true.
A short time later, some people were standing near Peter saying, “Surely you are one of those who followed Jesus, because you are from Galilee, too.”
71 Then Peter began to place a curse on himself and swear, “I don’t know this man you’re talking about!”
72 At once, the rooster crowed the second time. Then Peter remembered what Jesus had told him: “Before the rooster crows twice, you will say three times that you don’t know me.” Then Peter lost control of himself and began to cry.
Footnotes
- 14:24 new Some Greek copies do not have this word. Compare Luke 22:20.
- 14:25 fruit of the vine Product of the grapevine; this may also be translated “wine.”
- 14:36 Abba Name that a Jewish child called his father.
- 14:36 cup Jesus is talking about the terrible things that will happen to him. Accepting these things will be very hard, like drinking a cup of something bitter.
- 14:68 And the rooster crowed. Some Greek copies do not have this phrase.
© 2017 Bible League International
The Holy Bible, New Century Version®. Copyright © 2005 by Thomas Nelson, Inc.
