Petro akageuka na kumwona yule mfuasi mwingine aliyependwa sana na Yesu akitembea nyuma yao. (Huyu alikuwa ni mfuasi aliyejilaza kwa Yesu wakati wa chakula cha jioni na kusema, “Bwana, ni nani atakayekusaliti kwa maadui zako?”)
Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’