Ilikuwa baridi, hivyo watumishi na walinzi waliwasha moto wa kuni. Walikuwa wameuzunguka, wakipasha joto miili yao naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao.
Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa mkaa ambao walikuwa wamewasha kwa sababu pale ukumbini palikuwa na baridi kali. Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.