Lakini hivi ndivyo wengine hufikiri: Tunapotenda mabaya, inaonesha wazi kuwa Mungu ni wa haki. Je, tunaweza kusema kwamba Mungu hatutendei haki anapotuadhibu?
Lakini iwapo uovu wetu unadhihirisha wazi kwamba Mungu ni mwenye haki, tusemeje basi? Je, tuseme kuwa Mungu hana haki kutuadhibu? Hapa ninasema kibinadamu.