Kisha nikamwona Mwanakondoo amesimama katikati karibu na kiti cha enzi kilichozungukwa na viumbe wanne wenye uhai. Wazee pia walikuwa wamemzunguka Mwanakondoo aliyeonekana kama aliyeuawa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambayo ni roho saba za Mungu zilizotumwa ulimwenguni kote.
Katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wanne na wale wazee, nikaona Mwana- Kondoo amesimama, akionekana kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba, na macho saba, ambayo ni wale roho saba wa Mungu waliotumwa ulimwenguni kote .