Ufunuo 3:18
Print
Ninakushauri ununue dhahabu kutoka kwangu, dhahabu iliyosafishwa katika moto. Kisha utakuwa tajiri. Nakuambia hili: Nunua kwangu mavazi meupe. Ndipo utaweza kuifunika aibu ya uchi wako. Ninakuagiza pia ununue kwangu dawa ya kuweka kwenye macho yako, nawe utaweza kuona.
Kwa hiyo ninakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosaf ishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri; na mavazi meupe ili upate kuvaa, ufiche aibu ya uchi wako. Ujinunulie pia mafuta uyapake macho yako ili upate kuona.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica