Ufunuo 20:4
Print
Kisha nikaona viti vya enzi na watu wamevikalia. Hawa ni wale waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Na nikaona roho za wale waliouawa kwa sababu walikuwa waaminifu kwa kweli ya Yesu na ujumbe kutoka kwa Mungu. Hawakumwabudu mnyama wala sanamu yake. Hawakuipokea alama ya mnyama kwenye vipaji vya nyuso zao au mkononi mwao. Walifufuka na kutawala na Kristo kwa miaka elfu moja.
Kisha nikaona viti vya enzi. Na kwenye viti hivyo vya enzi waliketi wale waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Pia nikaona roho za wale watu waliokatwa vichwa kwa ajili ya kumshuhudia Yesu na kwa ajili ya neno la Mungu. Wao hawakuwa wamemwabudu yule mnyama wala sanamu yake na hawakuwa wamepokea alama ya yule mnyama kwenye vipaji vya nyuso zao wala mikononi mwao. Walifufuka kutoka kwa wafu wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu moja.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica