Yohana alikuja akiwaonesha njia sahihi ya kuishi, na hamkumwamini. Lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini Yohana. Mliona yaliyotokea, lakini hamkubadilika na mlikataa kumwamini.
Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumwamini, ila watoza ushuru na makahaba walimwamini. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kum wamini.”