Wakati wowote watakapowakamata na kuwashitaki, msiwe na wasiwasi kujiandaa kwa yale mtakayoyasema, lakini myaseme yale mtakayopewa saa ile ile, kwa kuwa si ninyi mnaozungumza; bali, ni Roho Mtakatifu anayezungumza.
“Mtakapokamatwa na kupelekwa mahakamani, msihangaike kuhusu mtakalosema. Semeni lo lote litakalowajia wakati huo, kwa sababu maneno mtakayosema si yenu bali yatatoka kwa Roho Mtaka tifu.