Luka 8:13
Print
Wengine wanafanana na mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye mawe. Ni watu ambao huyasikia mafundisho ya Mungu na kuyapokea kwa furaha, lakini kwa kuwa hawana mizizi yenye kina, huamini kwa muda mfupi. Majaribu yanapokuja, humwacha Mungu.
Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica