Lakini kabla ya mambo haya yote kutokea, watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Watawahukumu katika masinagogi yao na kuwafunga gerezani. Mtalazimishwa kusimama mbele ya wafalme na magavana. Watawatendea mambo haya yote kwa sababu ninyi ni wafuasi wangu.
“Lakini kabla haya yote hayajatokea watu watawakamata ninyi na kuwatesa. Mtashtakiwa mbele ya wakuu wa masinagogi na kufungwa magerezani; na wengine mtapelekwa kushtakiwa mbele ya wafalme na watawala kwa ajili ya jina langu.