Ndipo Yesu akajisikia furaha kwa uweza wa Roho Mtakatifu, akasema, “Ninakusifu wewe, Baba, BWANA wa mbingu na nchi. Ninashukuru kwamba umewaficha mambo haya wenye hekima na akili nyingi. Lakini umeyafunua kwa watu walio kama watoto wadogo. Ndiyo, Baba, umefanya hivi kwa sababu hakika ndivyo ulitaka kufanya.
Wakati huo, Yesu akiwa amejawa na furaha ya Roho Mtaka tifu, akasema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya ambayo umewaficha wenye elimu na wenye hekima umependa kuwafunulia wale wakuaminio kama watoto wadogo. Na haya yote yamefanyika kwa mapenzi yako Baba.