Mwanamke anapojifungua mtoto, hupata maumivu, kwa sababu wakati wake umefika. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa, huyasahau maumivu yale. Husahau kwa sababu huwa na furaha kwa kuwa mtoto amezaliwa ulimwenguni.
Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani.