Waebrania 12:1
Print
Tunao hawa watu mashuhuri wakituzunguka kama mifano kwetu. Maisha yao yanatueleza imani ni nini. Hivyo, nasi pia, tunapaswa kufanya mashindano yaliyo mbele yetu na kamwe tusikate tamaa. Tunapaswa kuondoa katika maisha yetu kitu chochote kitakachotupunguzia mwendo pamoja na dhambi zinazotufanya tutoke kwenye mstari mara kwa mara.
Basi na sisi kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa namna hii la mashahidi, tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi inay otusonga kwa urahisi; tupige mbio kwa ustahimilivu katika mashin dano yaliyowekwa mbele yetu.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) © 2017 Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica