Lakini mjane akiwa na watoto au wajukuu, jambo la kwanza ambalo wanahitaji kujifunza ni hili: kutimiza wajibu waliyonao kwa wanafamilia wao. Kwa kuwapa heshima na kuwahudumia, watakuwa wanawalipa fadhila wazazi wao na pia mababu na nyanya zao. Na haya ndiyo mambo yanaompendeza Mungu.
Kama mjane ana watoto ama wajukuu, hao watimize wajibu wao wa kidini kwa familia, kwa kuwahudumia wazazi na hivyo wawarudishie wema wal iowatendea. Kwa kufanya hivyo watampendeza Mungu.