Ikiwa kipawa chako ni kuhubiri, maneno yako yawe kama yanayotoka kwa Mungu. Ikiwa kipawa chako ni kuhudumu, unatakiwa kuhudumu kwa nguvu anazokupa Mungu. Ndipo Mungu atakaposifiwa kwa kila jambo katika Yesu Kristo. Uwezo na utukufu ni wake milele na milele. Amina.
Mtu akisema kitu, basi na awe kama anayesema maneno halisi ya Mungu. Mtu anayetoa huduma na ahudumu kwa nguvu apewayo na Mungu; ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye ni mwenye utukufu na uweza, milele na milele. Amina.