Majaribu mliyonayo ni yale yale waliyonayo watu wote. Lakini Mungu ni mwaminifu maana hataacha mjaribiwe kwa kiwango msichoweza kustahimili. Mnapojaribiwa, Mungu atawapa mlango wa kutoka katika jaribu hilo. Ndipo mtaweza kustahimili.
Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.