Font Size
Verse of the Day
A daily inspirational and encouraging Bible verse.
Duration: 366 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
1 Timotheo 2:1-2
Mungu Anataka Tumwombee Kila Mtu
2 Kwanza kabisa, ninakuagiza uwaombee watu wote. Uwaombee kwa Mungu ili awabariki na kuwapa mahitaji yao. Kisha umshukuru Yeye. 2 Unapaswa kuwaombea watawala na wote wenye mamlaka. Uwaombee viongozi hawa ili tuweze kuishi maisha yenye utulivu na amani, maisha yaliyojaa utukufu kwa Mungu na yanayostahili heshima.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International