Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Semicontinuous)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with sequential stories told across multiple weeks.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Exod for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 16:35-40

35 Asubuhi iliyofuata maofisa wa Kirumi waliwatuma baadhi ya askari kwenda gerezani na wakamwambia mkuu wa gereza, “Waachie watu hawa huru.”

36 Mkuu wa gereza akamwambia Paulo, “Maofisa wamewatuma askari hawa ili kuwaachia huru. Mnaweza kuondoka sasa. Nendeni kwa amani.”

37 Lakini Paulo akawaambia askari, “Wale maofisa hawakuthibitisha kuwa tulifanya chochote kibaya, lakini walitupiga kwa bakora hadharani na kutuweka gerezani. Nasi ni raia wa Rumi.[a] Na sasa wanataka tuondoke kimya kimya. Haiwezekani, ni lazima waje hapa wao wenyewe kisha watutoe nje!”

38 Askari wakawaambia maofisa alichosema Paulo. Waliposikia kwamba Paulo na Sila ni raia wa Rumi, waliogopa. 39 Hivyo walikwenda gerezani kuwaomba msamaha. Waliwatoa nje ya gereza na kuwaomba waondoke mjini. 40 Lakini Paulo na Sila walipotoka gerezani, walikwenda nyumbani kwa Lydia. Wakawaona baadhi ya waamini pale, wakawatia moyo. Kisha wakaondoka.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International