Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Mwogopeni Mungu, Siyo Watu
(Mt 10:28-31)
4 Kisha Yesu akawaambia watu, “Ninawaambia ninyi, rafiki zangu, msiwaogope watu. Wanaweza kuua mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya chochote cha kuwaumiza. 5 Mwogopeni Mungu maana Yeye ndiye mwenye nguvu ya kuwaua na kuwatupa Jehanamu. Ndiyo, mnapaswa kumwogopa yeye.
6 Ndege wanapouzwa, ndege watano wadogo wanagharimu senti mbili tu za shaba. Lakini Mungu hasahau hata mmoja wao. 7 Ndiyo, Mungu anajua hata idadi ya nywele mlizonazo kwenye vichwa vyenu. Msiogope ninyi ni wa thamani kuliko ndege wengi.
Msiionee Haya Imani Yenu
(Mt 10:32-33; 12:32; 10:19-20)
8 Ninawaambia, mkinikiri mbele za watu, ndipo nami[a] nitakiri kuwa ninyi ni wangu mbele za Mungu na malaika. 9 Na atakayenikataa mimi mbele za watu, nami nitamkataa mbele za Mungu na malaika.
10 Kila asemaye neno kinyume na Mwana wa Adamu atasamehewa. Lakini atakayesema kinyume na Roho Mtakatifu hatasamehewa.
11 Watakapowapeleka ninyi katika masinagogi mbele ya viongozi na wenye mamlaka, msihangaike mtasema nini. 12 Roho Mtakatifu atawafundisha wakati huo huo mnachopaswa kusema.”
© 2017 Bible League International