Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Semicontinuous)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with sequential stories told across multiple weeks.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Isa for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Amos for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Wakorintho 9

Msaada Kwa Ajili ya Watu wa Mungu

Kwa hakika sina haja ya kuwaandikia ninyi juu ya msaada huu kwa watu wa Mungu. Ninajua kuwa mnataka kusaidia. Nimekuwa ninajisifu sana juu yenu kwa watu wa Makedonia. Niliwaeleza kwamba ninyi watu wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana. Na shauku yenu ya kutoa zaidi imewafanya watu walio wengi zaidi hapa wawe tayari kutoa pia. Lakini ninawatuma kaka hawa kwenu. Sipendi kujisifia kwetu juu yenu kuthibitishwe kuwa ni batili. Nataka muwe tayari kama ambavyo nimesema kuwa mtakuwa tayari. Ikiwa baadhi ya Wamakedonia walio wengi wangefuatana nami na kuwakuta hamko tayari, tutaaibika. Tutaibika kwa kuwa tulikuwa na uhakika sana juu yenu. Na ninyi mtaaibika pia! Hivyo nikafikiri kuwa niwaombe ndugu hawa waje kwenu kabla ya mimi kuja. Wao watasaidia kufanya maandalizi mapema kwa ajili ya sadaka yenu yenye ukarimu mliyoahidi. Kisha sadaka hii itakuwa tayari tutakapokuja, na itaonekana kuwa baraka, na si kitu kidogo ambacho hamkutaka kutoa.

Kumbukeni hili: Yeye apandaye mbegu chache atapata mavuno kidogo. Lakini apandaye kwa wingi atapata mavuno mengi. Kila mmoja wenu atoe kama alivyo kusudia kutoa katika moyo wake. Hampaswi kutoa ikiwa mnajisia huzuni kufanya hivyo au ikiwa mnasikia kulazimishwa kutoa. Mungu anawapenda wale wanaotoa kwa furaha. Na Mungu anaweza kuwapeni baraka zaidi kuliko mlivyo katika kuhitaji kwenu, na daima mtakuwa na kila kitu mnachokihitaji. Mtakuwa na vingi vya ziada vya kutoa kwa kila kazi njema. Kama Maandiko yanavyosema,

“Hawakuwa na choyo waliwapa maskini.
    Mambo mema waliyoyafanya yatadumu millele.”(A)

10 Mungu ndiye huwapa mbegu wale wanaopanda, na anatoa mkate kuwa chakula. Na Mungu atawapeni “mbegu” na kuifanya ile mbegu ikue. Atazalisha mazao makubwa kutokana na wema wenu. 11 Mungu atawatajirisha katika namna zote ili mweze kutoa kwa uhuru kila mara. Na kutoa kwenu kulikosimamiwa na sisi kutawafanya watu wamshukuru Mungu.

12 Huduma mnayoitoa inawasaidia watu wa Mungu katika mahitaji yao, lakini si hayo tu itendayo. Inaleta pia shukrani nyingi zaidi na zaidi kwa Mungu. 13 Huduma hii ni uthibitisho wa imani yenu, na watu watamsifu Mungu kwa sababu kwa uhuru mlitoa mkawapa sehemu pamoja na watu wengine pia. Watamsifu Mungu kwa sababu wanaona jinsi mnavyoifuata injili ya Yesu Kristo ambayo mliipokea kwa wazi kabisa. 14 Na wanapoomba kwa ajili yenu, watatamani wangekuwa pamoja nanyi. Watajisikia hivi kwa sababu ya neema ya ajabu aliyowapa Mungu. 15 Mungu apewe shukrani kwa kipawa chake ambacho ni ajabu sana kukielezea.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International