Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
5 Usiseme kwa hasira kwa mtu mzima. Lakini sema naye kama baba yako. Watunze vijana kama kaka zako. 2 Watendee wanawake wazee kama mama zako. Na watendee wanawake vijana kwa heshima zote kama vile ni dada zako.
Kuwatunza Wajane
3 Watunze wajane ambao hasa wanahitaji msaada. 4 Lakini mjane akiwa na watoto au wajukuu, jambo la kwanza ambalo wanahitaji kujifunza ni hili: kutimiza wajibu waliyonao kwa wanafamilia wao. Kwa kuwapa heshima na kuwahudumia, watakuwa wanawalipa fadhila wazazi wao na pia mababu na nyanya zao. Na haya ndiyo mambo yanaompendeza Mungu. 5 Mjane ambaye hakika anahitaji msaada ni yule ambaye ameachwa pekee yake. Anamuamini Mungu kumtunza katika mahitaji yake. Anayemuomba msaada Mungu wakati wote. 6 Lakini mjane anayetumia maisha yake kujipenda ni hakika amekufa angali hai. 7 Wambie waumini huko kutunza familia zao wenyewe ili kwamba asiwepo yeyote atakayesema wanafanya vibaya. 8 Kila mtu atunze watu wa kwao, muhimu sana watunze familia zao. Kama hawatendi hayo watakuwa hawakubaliani na tunayoamini. Watakuwa wabaya kuliko hata asiyeamini.
© 2017 Bible League International