Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
17 Mtu akikukosea, usimlipize ubaya. Mjaribu kufanya lile ambalo kila mtu anaona kuwa ni sahihi. 18 Mjitahidi kadri mwezavyo kuishi kwa amani na kila mtu. 19 Rafiki zangu, msijaribu kumwadhibu yeyote anayewakosea. Msubiri Mungu katika hasira yake awaadhibu. Katika Maandiko Bwana anasema, “Nitawaadhibu wao kwa ajili ya yale waliyofanya.”(A) 20 Badala yake,
“ikiwa una adui wenye njaa,
wapeni chakula wale.
Ikiwa wana kiu,
wapeni kinywaji wanywe.
Kwa kufanya hivyo mtawafanya wajisikie aibu.”[a](B)
21 Msiruhusu uovu uwashinde, bali ushindeni uovu kwa kutenda mema.
Kuwapenda Wengine Ndiyo Sheria Pekee
8 Msidaiwe chochote na mtu, isipokuwa mdaiwe upendo baina yenu. Mtu anayewapenda wengine anakuwa amefanya yote yanayoamriwa na sheria. 9 Sheria inasema, “Usizini, usiue, usiibe, usitamani kitu cha mtu mwingine.”(A) Amri hizo zote na zingine hakika zinajumlishwa na kuwa kanuni moja tu, “Mpende jirani yako[a] kama unavyojipenda wewe mwenyewe.”(B) 10 Upendo hauwaumizi wengine. Hivyo kupenda ni sawa na kuitii sheria yote.
© 2017 Bible League International