Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Semicontinuous)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with sequential stories told across multiple weeks.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Job for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
1 Wakorintho 9:1-16

Haki Ambazo Paulo Hajazitumia

Mnajua kuwa mimi ni mtu niliye huru. Mnajua kuwa mimi ni mtume na kwamba nilimwona Yesu Bwana wetu. Na ninyi ni kielelezo cha kazi yangu katika Bwana. Wengine wanaweza wasikubali kuwa mimi ni mtume, lakini hakika ninyi mnakubali. Ninyi ni uthibitisho kuwa mimi ni mtume wa Bwana.

Ninataka kuwajibu baadhi ya watu wanaotaka kunichunguza. Je, hatuna haki ya kula na kunywa? Je, hatuna haki ya kusafiri pamoja na mke aliye mwamini? Mitume wengine wote, wadogo zake Bwana na Petro hufanya hivi. Na je, ni mimi na Barnaba tu ndiyo ambao ni lazima tufanya kazi ili tupate kipato cha kutuwezesha kuishi? Ni askari gani aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi la kondoo na hanywi maziwa?

Lakini nina mifano mingi kutoka katika maisha ya kila siku inayosisitiza hoja yangu. Sheria ya Mungu inasema vivyo hivyo pia. Ndiyo, imeandikwa katika Sheria ya Musa kuwa; “Mnyama wa kazi anapotumika kupura nafaka, usimzuie kula nafaka.”(A) Je, Mungu aliposema hivi, alikuwa anawawazia wanyama pekee? Hapana. 10 Hakika Mungu alizungumza kuhusu sisi. Ndiyo, iliandikwa kwa ajili yetu. Wote wawili, anayelima na anayepura nafaka, wana haki ya kupata nafaka kutokana na kazi yao. 11 Ikiwa tulipanda mbegu ya kiroho mioyoni mwenu, je, hatustahili kupata vitu kwa ajili ya maisha haya kutoka kwenu? 12 Ikiwa wengine wana haki ya kupata vitu kutoka kwenu, hakika hata sisi tuna haki pia. Lakini hatuitumii haki hii. Tunavumilia katika hali zote ili tusimfanye mtu yeyote akaacha kuitii Habari Njema ya Kristo. 13 Hakika mnajua ya kuwa wanaotumika Hekaluni hula chakula kutoka Hekaluni. Na wale wanaotumika madhabahuni hupata sehemu ya yale yanayotolewa madhabahuni. 14 Vivyo hivyo kwa wale wenye kazi ya kuhubiri Injili. Bwana ameamuru kuwa nao wataishi kutokana na kazi hiyo.

15 Lakini sijatumia haki hizi, na si kwamba ninataka kitu chochote kutoka kwenu. Ijapokuwa ninaandika hivi hilo si lengo langu. Ni bora nife kuliko mtu yeyote kuchukua kutoka kwangu kitu ninachojivunia. 16 Sijivuni kwa sababu ya kazi yangu ya kuhubiri Habari Njema kwa sababu ni wajibu wangu ambao ni lazima nifanye; ole wangu nisipowahubiri watu Habari Njema.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International