Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
29 Kaka zangu nina maana ya kuwa muda uliosalia ni mchache, wale waliooa waishi kama vile hawajaoa.[a] 30 Wale wanaolia wawe kama wasiolia, wenye furaha wawe kama hawana furaha na wale wanaonunua vitu wawe kama hawavimiliki vitu hivyo. 31 Vitumieni vitu vya ulimwengu pasipo kuviruhusu viwe vya muhimu kwenu. Hivi ndivyo mnapaswa kuishi, kwa sababu ulimwengu huu kwa namna ulivyo sasa, unapita.
Yesu Aanza Kazi yake Galilaya
(Mt 4:12-17; Lk 4:14-15)
14 Baada ya Yohana kuwekwa gerezani, Yesu akaja katika wilaya karibu na Ziwa Galilaya, huko aliwatangazia watu Habari Njema kutoka kwa Mungu. 15 Akasema, “Wakati umefika. Ufalme wa Mungu umewafikia.[a] Mbadili mioyo yenu na maisha yenu, na kuiamini habari njema!”
Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi
(Mt 4:18-22; Lk 5:1-11)
16 Alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa Galilaya, Yesu alimwona Simoni[b] na Andrea ndugu yake. Hao walikuwa wavuvi na walikuwa wakizitupa nyavu zao ziwani kukamata samaki. 17 Yesu akawaambia, “njooni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine, nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 18 Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata.
19 Kisha Yesu akaendelea mbele kidogo na akawaona ndugu wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na kaka yake Yohana. Yesu aliwaona wakiwa kwenye mashua wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. 20 Naye akawaita mara moja. Hivyo wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua na watu waliowaajiri na kumfuata Yesu.
© 2017 Bible League International