Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
5 Mungu kamwe hajamwambia malaika yeyote maneno haya:
“Wewe ni Mwanangu.
Mimi leo hii nimekuwa Baba yako.”(A)
Mungu pia kamwe hajasema juu ya malaika,
“Nitakuwa Baba yake,
naye atakuwa mwanangu.”(B)
6 Na kisha, pale Mungu anapomtambulisha Mwanaye mzaliwa wa kwanza ulimwenguni,[a] anasema,
“Basi malaika wote wa Mungu wamwabudu yeye.”[b]
7 Hivi ndivyo Mungu alivyosema kuhusu malaika:
8 Lakini hivi ndivyo alivyosema kuhusu Mwana wake:
“Mungu, ufalme wako utadumu milele na milele.
Unatumia mamlaka yako kwa haki.
9 Unapenda kilicho sahihi na kuchukia kilicho na makosa.
Hivyo Mungu, Mungu wako, amekuchagua wewe,
na amekupa heshima na furaha zaidi kupita yeyote aliye kama wewe.”(D)
10 Pia Mungu alisema,
“Ee Bwana, mwanzo uliiumba dunia,
na mikono yako ikaliumba anga.
11 Vitu hivi vitatoweka, lakini wewe utaendelea kuwepo.
Vyote vitachakaa kama mavazi makuu kuu.
12 Utavikunja hivyo kama koti,
navyo vitabadilishwa kama mavazi.
Lakini wewe hubadiliki,
na uhai wako hautafikia mwisho.”(E)
13 Na Mungu hakuwahi kusema haya kwa malaika:
14 Malaika wote ni roho ambao humtumikia Mungu nao hutumwa kuwasaidia wale watakaoupokea wokovu.
© 2017 Bible League International