Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
13 Pia, tunamshukuru Mungu pasipo kuacha kwa sababu ya namna mlivyoupokea ujumbe wake. Ingawa tuliuleta kwenu, mliupokea si kama ujumbe unaotoka kwa wanadamu, bali kama ujumbe wa Mungu. Kweli hakika ni ujumbe kutoka kwa Mungu, unaofanya kazi kwenu ninyi mnao uamini. 14 Kaka na dada zangu katika Bwana, mmeufuata mfano wa makanisa ya Mungu yaliyoko Uyahudi[a] yaliyo mali ya Kristo Yesu. Nina maana ya kuwa ninyi mlitendewa vibaya na watu wa kwenu, namna ile ile walioamini wa Kiyahudi walivyotendewa vibaya na Wayahudi wenzao. 15 Wayahudi wengine pia walimuua Bwana Yesu na manabii. Na walitulazimisha sisi kuondoka katika mji lenu. Hawampendezi Mungu, na wako kinyume na watu wengine wote. 16 Na wanajaribu kutuzuia tusizungumze na wasio Wayahudi. Wanapofanya hivi wanawazuia watu wasio Wayahudi kuokoka. Na hivyo wanaendelea kuziongeza dhambi zao hata kujaza kipimo. Sasa wakati umefika kwa wao kuadhibiwa na hasira ya Mungu.
Shauku ya Paulo kuwa tembelea tena
17 Kaka na dada zangu, tulikuwa kama yatima, tulitengwa nanyi kwa muda. Lakini hata kama hatukuwa pamoja nanyi, mawazo yetu yalikuwa bado yangali nanyi. Tulitamani sana kuwaona, na tulijitahidi sana kulitimiza hilo. 18 Ndiyo, tulitamani kuja kwenu. Mimi, Paulo, nilijaribu zaidi ya mara moja kuja kwenu, lakini Shetani alituzuia. 19 Ninyi ni tumaini letu, furaha yetu, na taji yetu tutakayojivunia wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu. 20 Mnatuletea heshima na furaha.
© 2017 Bible League International