Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Kazi ya Tito Krete
5 Nilikuacha kule Krete ili uweze kuyakamilisha yale yaliyokuwa yamebaki kufanyiwa kazi. Kisha nakuagiza uteue wazee na kuwaweka kuwa viongozi katika kila mji. 6 Anayeweza kuteuliwa ni yule ambaye halaumiwi kwa matendo yoyote mabaya, na aliye mwaminifu kwa mkewe,[a] na anao watoto wanaoamini Mungu[b] na ambao sio wakaidi. 7 Kwa sababu kila askofu,[c] anao wajibu wa kuitunza kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiyelaumiwa kwa kutenda mabaya yoyote. Asiwe mtu mkorofi. Asiwe mtu aliye mwepesi wa hasira. Asiwe mgomvi. Asiwe mtu mwenye kujipatia fedha toka kwa watu kwa njia ya udanganyifu. 8 Mzee anapaswa kuwa mtu anayewakaribisha watu nyumbani mwake. Anapaswa kuyapenda yaliyo mema. Azingatie kuishi maisha yaliyo matakatifu. Na awe na uwezo wa kudhibiti nafsi yake. 9 Anapaswa kuwa mwaminifu kwa ujumbe ule ule wa kweli tunaofundisha. Kwa namna hiyo ataweza kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya kweli na yenye manufaa.[d] Na ataweza kuwathibitishia wale wanaopinga mafundisho yake ya kuwa hawako sahihi.
10 Aina hii ya mafundisho ni muhimu kwa sababu wako watu wengi wasiopenda kumsikiliza mtu yeyote. Hao wanazungumzia mambo yao wenyewe yasiyo ya maana na kuwapotosha wengine waiache kweli. Ninaongelea hasa baadhi ya Wayahudi waaminio.[e] 11 Ni lazima wanyamazishwe kwani wanaivuruga jamii nzima kwa kufundisha mambo ambayo wasingepaswa kuyafundisha, lakini wanafanya hivyo ili kujipatia mapato yasiyo ya uaminifu! 12 Mmoja miongoni mwa watu wa kwao, Nabii kutoka Krete, alisema:
“Wakrete ni waongo daima.
Si bora kuliko wanyama wa porini.
Daima wapo tayari kula,
lakini hawapendi kufanya kazi.”
13 Usemi huu ni kweli, kwa hivyo wakaripie vikali ili wawe imara katika imani yao 14 na wasiendelee kuzisikilliza simulizi zinazopotosha za Kiyahudi na amri za wanadamu walioiacha kweli.
15 Kwa wale watu wenye mawazo yaliyo safi, kila kitu ni safi. Lakini hakuna kinachoweza kuwa safi kwa wasioamini ambao dhambi zao zimewafanya kuwa wachafu. Mawazo yao daima huwa yasiyo haki, na dhamiri zao pia zimekuwa chafu. 16 Hao hudai kuwa wanamjua Mungu, lakini matendo yao maovu yanaonesha kwa hakika kuwa hawamjui. Ni watu wenye kuchukiza mno na wasiotii, na hawafai kwa lo lote lililo jema.
© 2017 Bible League International