Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Kondoo wa Mungu
5 Sasa nina jambo la kuwaambia wazee walio katika kundi lenu. Mimi pia ni mzee nami mwenyewe nimeyaona mateso ya Kristo. Na nitashiriki katika utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Hivyo ninawasihi, 2 mlitunze kundi la watu mnalowajibika kwalo. Ni kundi lake Mungu.[a] Basi lichungeni kwa moyo wa kupenda na si kwa kulazimishwa. Hivi ndivyo Mungu anavyotaka. Fanyeni hivyo kwa sababu mnafurahi kutumika, na si kwa sababu mnataka pesa. 3 Msiwaongoze wale mnaowasimamia kwa kuwaamrisha. Lakini muwe mfano mzuri wa kuiga kwao. 4 Ili Kristo aliye Mchungaji Mkuu atakapokuja, mpate taji yenye utukufu na isiyopoteza uzuri wake.
5 Vijana, nina jambo la kuwaambia ninyi pia. Mnapaswa kutii mamlaka ya wazee. Na ninyi nyote mnapaswa kuwa wanyenyekevu ninyi kwa ninyi.
“Mungu yu kinyume na wanaojivuna,
lakini ni mwema kwa wanyenyekevu.”(A)
Salamu za Mwisho
12 Sila ataileta barua hii kwenu. Nafahamu kwamba ni ndugu mwaminifu katika familia ya Mungu. Niliandika barua hii fupi kuwatia moyo na kuwaambia kuwa hii ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
13 Kanisa lililoko Babeli[a] linatuma salamu kwenu. Wameteuliwa kama ninyi. Marko, ambaye ni kama mwanangu kwangu katika Kristo, anawasalimu pia. 14 Mpeni kila mmoja wenu salamu maalumu[b] mnapokutana.
Amani iwe kwenu ninyi nyote mlio katika Kristo.
© 2017 Bible League International