Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
17 Mtu anapokuwa ndani ya Kristo, anakuwa kiumbe[a] kipya kabisa. Mambo ya zamani yanakoma; na ghafla kila kitu kinakuwa kipya! 18 Yote haya yatoka kwa Mungu. Kupitia Kristo, Mungu alifanya amani katika yake na sisi. Na Mungu alitupa kazi ya kuleta amani kati ya watu na Mungu. 19 Tunachosema ni kuwa kupitia Kristo, Mungu alikuwa anaweka amani kati yake na ulimwengu. Alikuwa anatoa ujumbe wa msamaha kwa kila mtu kwa matendo mabaya waliyotenda kinyume naye. Na alitupa ujumbe huu wa amani ili kuwaeleza watu. 20 Hivyo tumetumwa kwa ajili ya Kristo. Ni kama Mungu anawaita watu kupitia sisi. Tunazungumza kwa niaba ya Kristo tunapowasihi ninyi kuwa na amani na Mungu. 21 Kristo hakuwa na dhambi,[b] ila Mungu alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu ili ndani ya Kristo tuweze kufanyika kielelezo cha wema wa uaminifu wa Mungu.
© 2017 Bible League International