Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Barua ya Yesu kwa Kanisa la Efeso
2 “Andika hivi kwa malaika[a] wa kanisa lililoko Efeso:
Huu ni ujumbe kutoka kwake yeye anayeshikilia nyota saba katika mkono wake wa kulia na kutembea katikati ya vinara vya taa saba vya dhahabu.
2 Ninayajua matendo yako, unavyofanya kazi kwa bidii na usivyokata tamaa. Ninajua kwamba huwakubali watu waovu. Umewajaribu wote wanaojiita mitume lakini si mitume. Umegundua kuwa ni waongo. 3 Huachi kujaribu. Umestahimili taabu kwa ajili ya jina langu na hujakata tamaa.
4 Lakini nina neno hili nawe umeuacha upendo uliokuwa nao hapo mwanzo. 5 Hivyo kumbuka ulipokuwa kabla ya kuanguka. Ugeuze moyo wako na utende yale uliyoyatenda mwanzoni. Usipobadilika, nitakuja kwako na kutoa kinara chako cha taa mahali pake. 6 Lakini unafanya vizuri kuyachukia matendo ya Wanikolai.[b] Mimi pia nayachukia mambo wanayotenda.
7 Kila anayesikia hili azingatie kile ambacho Roho anayaambia makanisa. Wale watakaoshinda, nitawapa haki ya kula matunda kutoka kwenye mti wa uzima, ulio katika Bustani ya Mungu.
© 2017 Bible League International