Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Mmechaguliwa kwa ajili ya Wokovu
13 Ndugu zangu, ninyi ni watu mnaopendwa na Bwana. Na imetupasa tumshukuru Mungu daima kwa sababu yenu. Hayo ndiyo tunayotakiwa kuyatenda, kwa sababu Mungu aliwaita kuwa miongoni mwa watu[a] wa kwanza kuokolewa. Mmeokolewa na Roho aliyewafanya muwe watu wa Mungu walio watakatifu kupitia kuiamini kweli. 14 Mungu aliwaita ninyi mpate wokovu. Aliwaita kwa kutumia Habari Njema tuliwahubiri. Mliitwa ili mshiriki katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15 Hivyo simameni imara na kuendelea kuamini mafundisho tuliyowapa tulipokuwa huko na kupitia barua yetu.
16-17 Tunaomba kwamba Bwana Yesu Kristo na Mungu Baba yetu awafariji na kuwaimairisha katika kila jambo jema mnalotenda na kusema. Mungu alitupenda na kutupa kupitia neema matumaini ya ajabu na faraja isiyo na mwisho.
Tuombee nasi
3 Na sasa, ndugu zangu, mtuombee. Ombeni kwamba mafundisho ya Bwana yaendelee kuenea haraka na kwamba watu watayaheshimu, kama ilivyotokea kwenu. 2 Mtuombee tupate ulinzi kutokana na watu wabaya na waovu. Mnafahamu, siyo wote wanamwamini Bwana.
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Atawapa nguvu na ulinzi dhidi ya Mwovu. 4 Tuna uhakika kwa sababu ya Bwana mnayemtumikia na mtaendelea kuyafanya yale tunayowaamuru. 5 Tunaomba kwamba Bwana atasababisha mjisikie upendo wa Mungu na kukumbuka subira ya ustahimilivu wa Kristo.
© 2017 Bible League International