Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
3 1-2 Nisingeweza kuja kwenu, ila ilikuwa vigumu kuendelea kusubiri zaidi. Hivyo tuliamua kumtuma Timotheo kwenu na tukabaki Athene peke yetu. Timotheo ni ndugu yetu. Ni mtenda kazi pamoja nasi kwa ajili ya Mungu katika kuwahubiri watu Habari Njema kuhusu Kristo. Nilimtuma Timotheo kuwaimarisha na kuwafariji katika imani yenu. 3 Tulimtuma ili asiwepo kati yenu atakayebugudhiwa na mateso tuliyo nayo sasa. Ninyi wenyewe mnatambua kuwa ni lazima tupatwe na mateso haya. 4 Hata pale tulipokuwa pamoja nanyi, tuliendelea kuwaeleza mapema ya kuwa sote tutapata matatizo. Na mnafahamu kuwa ilitokea kama tulivyowaambia. 5 Hii ndiyo sababu nilimtuma Timotheo kwenu, ili nipate kujua juu ya uaminifu wenu. Nilimtuma kwenu nilipokuwa siwezi kuendelea kusubiri zaidi. Nilihofu kuwa Shetani angeweza kuwashinda kwa majaribu yake. Kisha kazi yetu iliyokuwa ngumu ingepotea bure.
© 2017 Bible League International