Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
6 Daudi alisema mambo hayo hayo alipozungumzia baraka wanazopata watu pale Mungu anapowahesabia haki pasipo kuangalia matendo yao:
7 “Ni heri kwa watu
wanaposamehewa kutokana na mabaya waliyotenda,
dhambi zao zinapofutwa!
8 Ni heri kwa watu,
Bwana anapozifuta dhambi zao kutoka katika kumbukumbu yake!”(A)
9 Je, baraka hii ni kwa ajili ya waliotahiriwa tu? Au pia ni kwa ajili ya wale wasiotahiriwa? Tumekwisha sema ya kwamba Ibrahimu alikubaliwa kuwa ni mwenye haki mbele za Mungu kutokana na imani yake. 10 Sasa katika mazingira gani hili lilitokea? Je, Mungu alimkubali Ibrahimu na kumhesabia haki kabla au baada ya kutahiriwa? Mungu alimkubali kabla ya kutahiriwa kwake. 11 Ibrahimu alitahiriwa baadaye ili kuonesha kuwa Mungu amemkubali kuwa mwenye haki. Tohara yake ilikuwa uthibitisho kwamba Mungu alimhesabia haki kwa njia ya imani hata kabla ya kutahiriwa. Hivyo Ibrahimu ni baba wa wote wanaoamini lakini hawajatahiriwa. Kama Ibrahimu, wao pia wamekubaliwa na Mungu kuwa wenye haki kwa sababu ya imani yao tu. 12 Pia Ibrahimu ni baba wa waliotahiriwa, lakini si kwa sababu ya kutahiriwa kwao. Ni baba yao kwa sababu wao nao wamemwamini Mungu vile vile kama Ibrahimu alivyofanya kabla hajatahiriwa.
Ahadi ya Mungu Hupokelewa kwa Imani
13 Mungu aliweka ahadi kwa Ibrahimu na wazaliwa wake ya kuwapa ulimwengu wote. Lakini kwa nini Mungu aliweka ahadi hii? Haikuwa kwa sababu Ibrahimu aliifuata sheria. Ni kwa sababu aliiweka imani yake katika Mungu na akakubaliwa kuwa mwenye haki.
© 2017 Bible League International