Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
Yesu Kuhani Wetu Mkuu
8 Hii ndiyo hoja tunayosema: Tunaye kuhani mkuu wa jinsi hiyo, anayeketi upande wa kuume[a] wa kiti cha enzi cha Mungu Mkuu mbinguni. 2 Kuhani wetu mkuu anahudumia katika Patakatifu pa Patakatifu.[b] Anahudumia katika mahali pa hakika kwa ibada[c] palipotengenezwa na Bwana, siyo na mtu yeyote duniani.
3 Kila kuhani mkuu anayo kazi ya kutoa sadaka na sadaka kwa Mungu. Hivyo kuhani wetu mkuu pia anahitajika kutoa kitu kwa Mungu. 4 Kama kuhani wetu mkuu angekuwa anaishi duniani, asingekuwa kuhani. Nasema hivi kwa sababu tayari hapa wapo makuhani ambao wanafuata sheria kwa kutoa sadaka kwa Mungu. 5 Kazi ambayo makuhani hawa wanafanya hakika ni nakala tu na kivuli cha yaliyoko mbinguni. Ndiyo sababu Mungu alimwonya Musa alipokuwa amejiandaa kujenga Hema Takatifu: “Uwe na uhakika kufanya kila kitu sawasawa na kielelezo nilichokuonesha kule mlimani.”(A) 6 Lakini kazi ambayo tayari imetolewa kwa Yesu ni kuu zaidi ya kazi iliyotolewa na makuhani hao. Kwa jinsi hiyo hiyo, agano jipya ambalo Yesu alilileta kutoka kwa Mungu kuja kwa watu wake ni kuu zaidi kuliko lile la zamani. Na agano jipya limeelemea katika ahadi bora zaidi.
7 Kama kusingekuwa na makosa katika agano la kwanza, kisha kusingekuwa na haja ya agano la pili.
© 2017 Bible League International