Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
2 Rafiki yangu mpendwa, najua kwamba unaendelea vizuri kiroho, kwa hiyo ninaomba kuwa mengine yote yaendelee vizuri pia nawe uwe na afya njema. 3 Baadhi ya waamini walikuja na kunieleza juu ya kweli[a] iliyo katika maisha yako. Waliniambia kuwa unaendelea kuifuata njia ya kweli. Hili lilinifanya nijisikie furaha sana. 4 Daima hili hunipa furaha iliyo kuu ninaposikia kuwa wanangu wanaifuata njia ya kweli.
5 Rafiki yangu mpendwa, inapendeza kuwa unaonesha uaminifu wako katika kazi yako yote miongoni mwa waaminio. Wengine ambao huwajui. 6 Hao waliliambia kanisa juu ya upendo ulio nao. Tafadhali wasaidie kuendelea na safari yao. Wasaidie katika njia ambayo itampendeza Mungu. 7 Safari hiyo waliyoenda ni ya kumtumikia Kristo. Hawakupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. 8 Hivyo inatupasa kuwasaidia. Tunapowasaidia, tunashiriki kazi yao katika ile kweli.
© 2017 Bible League International