Revised Common Lectionary (Complementary)
4 Chochote kilichoandikwa zamani kiliandikwa ili kitufundishe sisi. Maandiko haya yaliandikwa ili yatupe matumaini yanayokuja kwa njia ya subira na kutia moyo kunakoletwa nayo. 5 Subira na kuhimiza kote hutoka kwa Mungu. Na ninawaombea ili Mungu awasaidie muwe na nia ile ile ninyi kwa ninyi, kama ilivyo nia ya Kristo Yesu. 6 Kisha ninyi nyote, kwa sauti moja, mtamtukuza Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. 7 Kristo aliwakaribisha ninyi, hivyo nanyi mkaribishane ninyi kwa ninyi. Hili litaleta heshima[a] kwa Mungu. 8 Ndiyo, haya ndiyo maneno yangu kwenu kwamba Kristo alifanyika mtumishi wa Wayahudi ili kuonesha kuwa Mungu amefanya yale aliyowaahidi baba zao wakuu. 9 Na pia alifanya hivi ili wale wasio Wayahudi waweze kumsifu Mungu kwa rehema anazowapa. Maandiko yanasema,
“Hivyo nitakushukuru wewe katikati ya watu wa mataifa mengine;
Nitaliimbia sifa jina lako.”(A)
10 Na Maandiko yanasema,
“Ninyi watu wa mataifa mengine furahini pamoja na watu wa Mungu.”(B)
11 Pia Maandiko yanasema,
“Msifuni Bwana ninyi watu wote wa mataifa mengine;
watu wote na wamsifu Bwana.”(C)
12 Na Isaya anasema,
“Mtu mmoja atakuja kutoka katika ukoo wa Yese.[b]
Atainuka na kutawala juu ya mataifa,
na wataweka matumaini yao kwake.”(D)
13 Naomba kwamba Mungu aletaye matumaini awajaze furaha na amani kadri mnavyomwamini yeye. Na hii isababishe tumaini lenu liongezeke hadi lifurike kabisa ndani yenu kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Yohana Atayarisha Njia kwa Ajili ya Yesu
(Mk 1:1-8; Lk 3:1-9,15-17; Yh 1:19-28)
3 Baadaye, kabla ya miaka mingi kupita, Yohana Mbatizaji alianza kuwahubiri watu ujumbe uliotoka kwa Mungu. Naye alihubiri kutokea maeneo ya nyikani huko Uyahudi. 2 Yohana alisema, “Tubuni na kuibadili mioyo yenu, kwa sababu ufalme wa Mungu umekaribia.” 3 Nabii Isaya alisema kuhusu habari za Yohana Mbatizaji pale aliposema,
“Kuna mtu anayeipaza sauti yake toka nyikani:
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana;
nyoosheni njia kwa ajili yake.’”(A)
4 Huyo Yohana alivaa mavazi yaliyofumwa kutokana na manyoya ya ngamia. Naye alijifunga mkanda wa ngozi kuzunguka kiuno chake, na alikula nzige na asali mbichi. 5 Watu kutoka Yerusalemu na maeneo yote ya Uyahudi na wale kutoka maeneo yote yaliyo kando ya Mto Yordani walikwenda kwa Yohana Mbatizaji; 6 huko waliungama matendo yao mabaya kwake naye akawabatiza katika Mto Yordani.
7 Mafarisayo na Masadukayo wengi walikwenda kwa Yohana ili wabatizwe. Yohana alipowaona, akasema, “Enyi ninyi nyoka! Ni nani amewaonya kuikimbia hukumu ya Mungu inayokuja? 8 Muibadili mioyo yenu! Na muoneshe kwa vitendo kuwa mmebadilika. 9 Ninajua mnachofikiri. Mnataka akasema kuwa, ‘lakini Ibrahimu ni baba yetu!’ Hiyo haijalishi. Ninawaambia Mungu anaweza kumzalia Ibrahimu watoto kutoka katika mawe haya. 10 Shoka limewekwa tayari kukata shina la mti katika mizizi yake. Kila mti[a] usiozaa matunda mazuri utakatwa vivyo hivyo na kutupwa motoni.
11 Mimi ninawabatiza kwa maji kuonesha kuwa mmebadilika mioyoni mwenu na pia maishani mwenu. Lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Naye atakuja akiwa tayari kwa ajili ya kuisafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri kutoka kwenye makapi,[b] na kisha ataiweka nafaka nzuri kwenye ghala yake. Kisha atayachoma makapi kwa moto usiozimika.”
© 2017 Bible League International