Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Complementary)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with thematically matched Old and New Testament readings.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: 2Sam for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Wathesalonike 1:3-12

Kaka na dada zetu, tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu. Na hivyo ndivyo tunavyopaswa kufanya, kwani mnatupa sababu ya kushukuru na imani yenu inakua zaidi na zaidi. Pamoja na hilo upendo ambao kila mmoja wenu anao kwa mwenzake nao unakua. Hivyo tunayaeleza makanisa mengine ya Mungu namna tunavyojivuna kuhusu ninyi. Tunawaeleza jinsi mlivyoendelea kwa subira kuwa imara na waaminifu, ingawa mnateswa na kusumbuliwa na matatizo mengi.

Mungu Atafanya Mambo Kuwa Sawa

Huu ni uthibitisho kwamba Mungu ni wa haki katika hukumu zake. Hutaka kuwastahilisha katika ufalme wake. Kuteswa kwenu ni kwa ajili ya ufalme huo. Ni haki kwa Mungu kuwaadhibu wale wanaowaletea matatizo. Atawaletea unafuu wanaoteseka. Atawaletea ninyi nasi unafuu huo atakapokuja Bwana Yesu kutoka mbinguni ili wote wamwone, pamoja na malaika wake wenye nguvu zilizotukuka. Atakuja na moto unaoteketeza kuwaadhibu wasiomjua Mungu na wanaokataa kuitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. Wataadhibiwa na maangamizi yasio na mwisho. Hawataruhusiwa kuwa na Bwana lakini watatengwa mbali na nguvu zake za utukufu. 10 Hii itatokea siku ambapo Bwana Yesu atakuja na kupokea heshima miongoni mwa watu wake watakatifu. Na wote wanaomwamini watamstaajabu. Na hii inawajumuisha ninyi kwa sababu mliamini yale tuliyowaambia.

11 Hii ndiyo sababu daima tunawaombea. Tunamwomba Mungu wetu awasaidie kuishi katika njia njema aliyoitaka alipowachagua. Wema mlionao unawafanya mtake kufanya mema. Na imani mliyonayo inafanya mfanye kazi. Tunaomba kwamba kupitia nguvu zake Mungu atayakamilisha yote mema mliyokusudia kufanya pamoja na kazi zote zinazotokana na imani yenu. 12 Kisha jina la Bwana wetu Yesu litaheshimiwa kwa sababu yenu, nanyi mtaheshimiwa kwa sababu yake, na mtaheshimiwa kwa sababu yake. Hii inaweza kutokea tu kwa neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International