Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Complementary)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with thematically matched Old and New Testament readings.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Deut for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Matendo 22:22-23:11

22 Watu waliacha kusikiliza Paulo aliposema jambo hili la mwisho. Walipasa sauti wote, wakisema, “Mwondosheni mtu huyu! Hastahili kuishi katika dunia hii tena.” 23 Waliendelea kupiga kelele, wakichana nguo zao na kurusha mavumbi juu.[a] 24 Ndipo kamanda akawaambia askari wamwingize Paulo kwenye jengo la jeshi na wampige. Alitaka kumlazimisha Paulo aeleze ni kwa nini watu walikuwa wanampigia kelele namna ile. 25 Askari walipokuwa wanamfunga Paulo, wakijiandaa kumpiga alimwuliza ofisa wa jeshi, “Je, mna haki ya kumpiga raia wa Rumi[b] ambaye hajathibitika kuwa na hatia?”

26 Ofisa aliposikia hili, alikwenda kwa kamanda na kumwambia. Ofisa alisema, “Unafahamu unalolifanya? Mtu huyu ni raia wa Rumi!”

27 Kamanda akaenda kwa Paulo na kusema, “Niambie kwa hakika, ‘Je, wewe ni raia wa Rumi?’”

Paulo akajibu, “Ndiyo.”

28 Kamanda akasema, “Nililipa pesa nyingi kuwa raia wa Rumi.”

Lakini Paulo akasema, “Nilizaliwa raia wa Rumi.”

29 Ghafla watu waliokuwa wanajiandaa kumwuliza maswali Paulo waliondoka. Kamanda aliogopa kwa sababu alikuwa ameshamfunga Paulo kwa minyororo na ni raia wa Rumi.

Paulo Aongea na Viongozi wa Kiyahudi

30 Siku iliyofuata kamanda alitaka kujua ni kwa nini Wayahudi wanamshitaki Paulo. Hivyo aliamuru viongozi wa makuhani na baraza kuu lote kukutana pamoja. Alimfungua Paulo minyororo na kumleta mbele ya baraza.

23 Paulo aliwatazama wajumbe wa baraza na kusema, “Ndugu zangu, Nimeishi maisha yangu katika njia nzuri mbele za Mungu. Daima nimefanya yale niliyodhani ni haki.” Anania,[c] kuhani mkuu alikuwa pale. Aliposikia hili, aliwaambia watu waliokuwa wamesisima karibu na Paulo wampige kwenye mdomo. Paulo akamwambia Anania, “Mungu atakupiga wewe pia! Wewe ni kama ukuta mchafu uliopakwa rangi nyeupe. Umeketi hapa na kunihukumu, ukitumia Sheria ya Musa. Lakini unawaambia wanipige wakati ni kinyume cha sheria.”

Watu waliokuwa wamesimama karibu na Paulo wakamwambia, “Una uhakika unataka kumtukana kuhani mkuu wa Mungu namna hiyo?”

Paulo akasema, “Ndugu zangu, sikufahamu kuwa mtu huyu ni kuhani mkuu. Maandiko yanasema, ‘Usiseme mambo mabaya kuhusu kiongozi wa watu wako.’”(A)

Paulo alijua kuwa baadhi ya watu kwenye baraza lile ni Masadukayo na baadhi yao ni Mafarisayo. Hivyo akapaza sauti akasema, “Ndugu zangu, Mimi ni Farisayo na baba yangu ni Farisayo! Nimeshitakiwa hapa kwa sababu ninaamini kuwa watu watafufuka kutoka kwa wafu.”

Paulo alipolisema hili, mabishano makubwa yakaanza kati ya Mafarisayo na Masadukayo. Baraza likagawanyika. (Masadukayo hawaamini katika ufufuo, malaika au roho. Lakini Mafarisayo wanaamini vyote.) Wayahudi hawa wote wakaanza kubishana kwa kupaza sauti. Baadhi ya walimu wa sheria, waliokuwa Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hatuoni kosa lolote kwa mtu huyu. Inawezekana kwa hakika malaika au roho alizungumza naye.”

10 Mabishano yaligeuka kuwa mapigano na kamanda aliogopa kwamba Wayahudi wangempasua Paulo vipande vipande. Hivyo akawaambia askari wateremke, wamwondoe Paulo na kumweka mbali na Wayahudi hao katika jengo la jeshi.

11 Usiku uliofuata Bwana Yesu akaja na kusimama pembeni mwa Paulo. Akamwambia, “Uwe jasiri! Umewaambia watu kuhusu mimi humu Yerusalemu. Ni lazima ufanye vivyo hivyo Rumi.”

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International