Revised Common Lectionary (Complementary)
Maelekezo ya Mwisho
10 Ninyi hata hivyo mmeyazingatia na kuyashika mafundisho yangu, mwenendo wangu na kusudi langu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu na ustahimilivu wangu, 11 mateso yangu na taabu zangu. Mnayajua mambo yaliyonitokea kule Antiokia, Ikonia, na Listra, mateso ya kutisha niliyoyastahimili! Lakini Bwana akaniokoa kutoka katika hayo yote. 12 Kwa hakika wote wanaoishi maisha yenye kumtukuza Mungu kama wafuasi wa Kristo Yesu watasumbuliwa. 13 Lakini watu waovu na wanaodanganya wengine wataendelea kuwa wabaya zaidi. Watawadaganya wengine na wao pia watajidanganya wenyewe.
14 Lakini imekupasa wewe kuendelea kuyashika mambo yale uliyojifunza na kuyathibitisha moyoni mwako kuwa ni ya kweli. Wewe unawajua na unawaamini wale waliokufundisha. 15 Na unajua kwamba umeyajua Maandiko Matakatifu tangu ukiwa mtoto. Maandiko hayo yana uwezo wa kukupa hekima. Hekima hiyo itakuongoza hadi kwenye wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
© 2017 Bible League International