Revised Common Lectionary (Complementary)
Mtu Tajiri Akataa Kumfuata Yesu
(Mk 10:17-31; Lk 18:18-30)
16 Mtu mmoja alimwendea Yesu na kumwuliza, “Mwalimu, nifanye jambo gani lililo jema ili niweze kuupata uzima wa milele?”
17 Yesu akajibu, “Kwa nini unaniuliza kuhusu jambo gani lililo jema? Mungu pekee yake ndiye mwema. Lakini ikiwa unataka kuupata uzima wa milele, zitii amri.”
18 Yule mtu akauliza, “Amri zipi?”
Yesu akajibu, “‘Usiue, usizini, usiibe, usiseme uongo, 19 mheshimu baba na mama yako,’(A) na ‘mpende jirani yako[a] kama unavyojipenda wewe mwenyewe.’”(B)
20 Yule kijana akasema, “Ninazitii amri hizi zote. Nifanye nini zaidi?”
21 Yesu akajibu, “Ikiwa unataka kuwa mkamilifu, nenda ukauze kila kitu unachomiliki. Uwape pesa maskini na utakuwa na utajiri mbinguni. Kisha njoo unifuate!”
22 Lakini kijana aliposikia Yesu anamwambia kuhusu kugawa pesa yake, alihuzunika. Hakutaka kufanya hivi kwa kuwa alikuwa tajiri sana. Hivyo aliondoka.
© 2017 Bible League International