Revised Common Lectionary (Complementary)
8 Lakini rafiki zangu wapendwa msisahau jambo hili moja ya kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu moja, na miaka elfu moja ni kama siku moja. 9 Bwana hakawii kufanya alichoahidi kama ambavyo watu wengine wanaelewa maana ya kukawia. Lakini Bwana amewavumilia. Hataki mtu yeyote aangamie. Anataka kila mtu abadili njia zake na aache kutenda dhambi.
10 Lakini siku atakayorudi Bwana itakuwa siku isiyotarajiwa na kila mtu kama ambavyo mwizi huja. Anga itatoweka kwa muungurumo wa sauti kuu. Kila kitu kilicho angani kitateketezwa kwa moto. Na dunia na kila kitu kilichofanyika ndani yake kitafunuliwa na kuhukumiwa[a] na Mungu. 11 Kila kitu kitateketezwa kwa namna hii. Sasa mnapaswa kuishi kwa namna gani? Maisha yenu yanapaswa kuwa matakatifu na yanayompa heshima Mungu. 12 Mnapaswa kuangalia mbele, kuiangalia siku ile ya Bwana, mkifanya kile mnachoweza ili ije mapema. Itakapofika, anga itateketezwa kwa moto na kila kitu kilicho angani kitayeyuka kwa joto. 13 Lakini Mungu alituahidi. Na tunasubiri alichoahidi, yaani anga mpya na dunia mpya. Mahali ambapo hakia unaishi.
© 2017 Bible League International