Revised Common Lectionary (Complementary)
Yesu Aingia Yerusalemu Kama Mfalme
(Mt 21:1-11; Mk 11:1-11; Yh 12:12-19)
28 Baada ya Yesu kusema mambo haya, aliendelea kusafiri kuelekea Yerusalemu. 29 Akakaribia Bethfage na Bethania, miji iliyo karibu na kilima kinachoitwa Mlima wa Mizeituni. Kisha akawatuma wawili miongoni mwa wafuasi wake, 30 akawaambia, “Nendeni kwenye mji mnaoweza kuuona pale. Mtakapoingia mjini, mtamwona mwanapunda amefungwa ambaye bado mtu yeyote hajampanda. Mfungueni na mleteni hapa kwangu. 31 Kama mtu yeyote akiwauliza, ‘Kwa nini mnamfungua?’ Semeni, ‘Bwana anamhitaji.’”
32 Wafuasi wawili wakaenda kwenye mji ule. Wakamwona punda kama Yesu alivyowaambia. 33 Wakamfungua, lakini wamiliki wa punda wakatoka. Wakawauliza wafuasi wa Yesu, “Kwa nini mnamfungua punda wetu?”
34 Wafuasi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” 35 Hivyo wafuasi wakampeleka punda kwa Yesu. Wakatandika baadhi ya nguo zao juu ya mwanapunda, kisha wakampandisha Yesu juu yake. 36 Yesu akaanza kwenda Yerusalemu. Wafuasi walikuwa wanatandaza nguo zao njiani mbele yake.
37 Yesu alipokaribia Yerusalemu. Alipokuwa katika njia inayotelemka kutoka kwenye Mlima wa Mizeituni, kundi lote la wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa kupaza sauti. Walimsifu Mungu kwa furaha kwa sababu ya miujiza yote waliyoiona. 38 Walisema,
“Karibu! Mungu ambariki mfalme
ajaye kwa jina la Bwana!(A)
Amani iwe mbinguni,
na utukufu kwa Mungu!”
39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika kundi wakamwambia Yesu, “Mwalimu, waambie wafuasi wako wasiseme mambo haya!”
40 Lakini Yesu akawajibu, “Ninawaambia ikiwa wafuasi wangu wasingesema, mawe haya yangesema kwa kupaza sauti!”
5 Hivi ndivyo mnapaswa kufikiri, kuhisi na kutenda katika maisha yenu kwa pamoja, kama vile Kristo Yesu alivyofikiri:
6 Alikuwa sawa na Mungu katika namna zote,
lakini hakufikiri kwamba kuwa sawa na Mungu
kilikuwa kitu cha manufaa kwake.
7 Badala yake, aliacha kila kitu,
hata sehemu yake pamoja na Mungu.
Akakubali kuwa kama mtumwa,
akiwa katika umbo la binadamu.
Wakati wa maisha yake kama mtu,
8 Alijinyenyekeza na akawa mtiifu kabisa kwa Mungu,
hata jambo hilo liliposababisha kifo chake msalabani.
9 Hivyo ndiyo sababu Mungu alimpa mahali pa heshima sana,
na akampa jina lililo kuu kuliko majina yote.
10 Hivyo kila mtu atasujudu kumheshimu Yesu.
Kila mmoja aliye mbinguni, duniani na wale walio chini ya dunia.
11 Wote watakiri kwamba, “Yesu Kristo ni Bwana,”
na hili litamtukuza Mungu Baba.
Chakula cha Bwana
(Mt 26:26-30; Mk 14:22-26; 1 Kor 11:23-25)
14 Wakati ulifika kwa wao kula mlo wa Pasaka. Yesu na mitume walikuwa wamekaa pamoja kuzunguka meza ya chakula. 15 Yesu akawaambia, “Nilitaka sana kula mlo huu wa Pasaka pamoja nanyi kabla sijafa. 16 Sitakula mlo mwingine wa Pasaka mpaka itakapopewa maana yake kamili katika ufalme wa Mungu.”
17 Kisha Yesu akachukua kikombe kilichokuwa na divai. Akamshukuru Mungu, na akasema, “Chukueni kikombe hiki na kila mmoja anywe. 18 Sitakunywa divai tena mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja.”
19 Kisha akaichukua baadhi ya mkate na akamshukuru Mungu. Akaigawa vipande vipande, akawapa vipande mitume na kusema, “Mkate huu ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili yenu. Kuleni kwa kunikumbuka.” 20 Katika namna ile ile, baada ya kula chakula, Yesu akachukua kikombe chenye divai na akasema, “Divai hii inawakilisha Agano Jipya kutoka kwa Mungu kwa watu wake. Litaanza pale damu yangu itakapomwagika kwa ajili yenu.”[a]
Nani Atamsaliti Yesu?
21 Yesu akasema, “Lakini hapa mezani kuna mkono wa yule atakayenisaliti kwa adui zangu. 22 Mwana wa Adamu atakufa kama Mungu alivyoamua. Lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe.”
23 Ndipo mitume wakaulizana, “Ni nani miongoni mwetu atafanya hivyo?”
Iweni Kama Mtumishi
24 Baadaye, mitume wakaanza kubishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu. 25 Lakini Yesu akawaambia, “Wafalme wa mataifa wanawatawala watu kama watumwa wao, na wenye mamlaka juu ya wengine wanataka kuitwa, ‘Wafadhili Wakuu’. 26 Lakini ni lazima msiwe hivyo. Aliye na mamlaka zaidi miongoni mwenu lazima awe kama asiye na mamlaka. Anayeongoza anapaswa kuwa kama anayetumika. 27 Nani ni mkuu zaidi: Yule anayetumika au yule aliyekaa mezani na kuhudumiwa? Kila mtu hudhani ni yule aliyekaa mezani akihudumiwa, sawa? Lakini nimekuwa pamoja nanyi kama ninayetumika.
28 Na ninyi ndiyo mliobaki pamoja nami katika mahangaiko mengi. 29 Hivyo ninawapa mamlaka kutawala pamoja nami katika ufalme ambao Baba yangu amenipa. 30 Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme huo. Mtakaa katika viti vya enzi na kuwahukumu makabila kumi na mbili ya Israeli.
Petro Atajaribiwa na Kushindwa
(Mt 26:31-35; Mk 14:27-31; Yh 13:36-38)
31 Shetani ameomba ili awapepete kwa nguvu kama mkulima anavyopepeta ngano kwenye ungo ili mwanguke. Simoni, Simoni,[b] 32 nimekuombea ili usipoteze imani yako! Wasaidie ndugu zako kuwa imara utakaponirudia.”
33 Lakini Petro akamwambia Yesu, “Bwana, niko tayari kufungwa gerezani pamoja nawe. Hata kufa pamoja nawe!”
34 Lakini Yesu akasema, “Petro, asubuhi kabla jogoo hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.”
Iweni Tayari kwa Matatizo
35 Kisha Yesu akawaambia mitume, “Kumbukeni nilipowatuma bila pesa, mkoba, wala viatu. Je, mlipungukiwa chochote?”
Mitume wakajibu, “Hapana.”
36 Yesu akawaambia, “Lakini sasa kama una pesa au mkoba, uchukue pamoja nawe. Kama huna upanga, uza koti lako ukanunue. 37 Maandiko yanasema, ‘Alidhaniwa kuwa mhalifu.’(A) Maandiko haya lazima yatimizwe. Yaliyoandikwa kuhusu mimi yanatimilika sasa.”
38 Wafuasi wakasema, “Tazama Bwana, hapa kuna panga mbili.”
Yesu akawaambia, “Nyamazeni, acheni mazungumzo ya namna hiyo!”
Yesu Aomba Akiwa Peke Yake
(Mt 26:36-46; Mk 14:32-42)
39-40 Yesu akaondoka mjini akaenda Mlima wa Mizeituni. Wafuasi wake wakaenda pamoja naye. (Alikuwa akienda huko mara kwa mara.) Akawaambia wafuasi wake, “Ombeni ili mtiwe nguvu msije mkajaribiwa.”
41 Kisha Yesu akaenda kama hatua hamsini mbali nao. Akapiga magoti na akaomba akisema, 42 “Baba, ukiwa radhi, tafadhali usinifanye ninywe katika kikombe[c] hiki. Lakini fanya unalotaka wewe, siyo ninalotaka mimi.” 43 Kisha malaika kutoka mbinguni akaja akamtia nguvu. 44 Yesu aliomba kwa nguvu zaidi na kustahimili zaidi kama mpiganaji wa mieleka akiwa katika mapambano makali. Jasho kama matone ya damu likadondoka kutoka kwenye uso wake.[d] 45 Alipomaliza kuomba, alikwenda kwa wafuasi wake. Akawakuta wamelala, wamechoka kwa sababu ya huzuni. 46 Yesu akawaambia, “Kwa nini mnalala? Amkeni, ombeni mtiwe nguvu msije mkajaribiwa.”
Yesu Akamatwa
(Mt 26:47-56; Mk 14:43-50; Yh 18:3-11)
47 Yesu alipokuwa anaongea, kundi likaja. Lilikuwa linaongozwa na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili. Akamwendea Yesu ili ambusu.
48 Lakini Yesu akamwambia, “Yuda unatumia busu la urafiki kumsaliti Mwana wa Adamu kwa adui zake?” 49 Wafuasi wa Yesu walikuwa wamesimama pale pia. Walipoona kilichokuwa kinatokea, wakamwambia Yesu, “Bwana, tutumie panga zetu?” 50 Na mmoja wao akautumia upanga wake. Akakata sikio la kulia la mtumishi wa kuhani mkuu.
51 Yesu akasema, “Acha!” Kisha akaligusa sikio la mtumishi na akamponya.
52 Yesu akaliambia lile kundi lililokuja kumkamata. Walikuwa viongozi wa makuhani, viongozi wa wazee wa Kiyahudi na askari walinzi wa Hekalu. Akawaambia, “Kwa nini mmekuja hapa mkiwa na mapanga na marungu? Mnadhani mimi ni mhalifu? 53 Nilikuwa pamoja nanyi kila siku katika eneo la Hekalu. Kwa nini hamkujaribu kunikamata pale? Lakini sasa ni wakati wenu, wakati ambao giza linatawala.”
Petro Amkana Yesu
(Mt 26:57-58,69-75; Mk 14:53-54,66-72; Yh 18:12-18,25-27)
54 Walimkamata Yesu na kumpeleka nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro alimfuata Yesu lakini alikaa nyuma kwa mbali. 55 Baadhi ya watu walikoka moto katikati ya ua kisha wakaketi pamoja. Petro naye aliketi pamoja nao. 56 Kutokana na mwanga wa moto, mtumishi wa kike alimwona Petro amekaa pale. Akamtazama Petro usoni kwa makini. Kisha akasema, “Huyu pia alikuwa na yule mtu.”
57 Lakini Petro akasema si kweli. Akasema, “Mwanamke, simfahamu mtu huyo!” 58 Muda mfupi baadaye, mtu mwingine akamwona Petro na akasema, “Wewe pia ni mmoja wa lile kundi!”
Lakini Petro akasema, “Wewe, mimi si mmoja wao!”
59 Baada ya kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasema, “Ni kweli, nina uhakika mtu huyu alikuwa pamoja naye, kwa sababu yeye pia anatoka Galilaya.”
60 Lakini Petro akasema, “Wewe, wala sijui unazungumza kuhusu nini!”
Alipokuwa bado anazungumza, jogoo aliwika. 61 Bwana aligeuka akamtazama Petro kwenye macho yake. Kisha Petro akakumbuka Bwana alivyokuwa amesema ya kwamba, “Kabla ya jogoo kuwika asubuhi, utakuwa umenikana mara tatu.” 62 Kisha Petro akatoka nje na kulia kwa uchungu.
Walinzi Wamdhalilisha Yesu
(Mt 26:67-68; Mk 14:65)
63 Walinzi waliokuwa wanamlinda Yesu walimfanyia mizaha na kumpiga. 64 Wakayafunika macho yake ili asiwaone. Kisha wakampiga na wakasema, “Tabiri, tuambie nani amekupiga!” 65 Walimtukana pia matusi ya kila aina.
Yesu Akiwa Mbele ya Viongozi wa Kidini
(Mt 26:59-66; Mk 14:55-64; Yh 18:19-24)
66 Alfajiri, viongozi wazee wa watu, viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikusanyika. Walimpeleka Yesu kwenye baraza lao kuu. 67 Wakamwambia, “Tuambie ikiwa wewe ni Masihi.”
Yesu akawaambia, “Hamtaniamini ikiwa nitawaambia kuwa mimi ni Masihi. 68 Na ikiwa nitawauliza swali, hakika mtakataa kunijibu. 69 Lakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu atakaa upande wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”
70 Wote wakasema, “Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Mnaweza kusema kuwa mimi ni Mwana wa Mungu.”
71 Wakasema, “Je, tunahitaji mashahidi wengine zaidi? Sote tumesikia alichosema yeye mwenyewe!”
Gavana Pilato Amhoji Yesu
(Mt 27:1-2,11-14; Mk 15:1-5; Yh 18:28-38)
23 Kisha kundi lote likasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2 Wakaanza kumshitaki Yesu na kumwambia Pilato, “Tumemkamata mtu huyu akijaribu kuwapotosha watu wetu. Anasema tusilipe kodi kwa Kaisari. Anajiita Masihi, mfalme.”
3 Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
Yesu akajibu, “Ndiyo, unaweza kusema hivyo.”
4 Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na watu, “Sioni kosa lolote kwa mtu huyu.”
5 Lakini waliendelea kusema, “Mafundisho yake yanasababisha matatizo katika Uyahudi yote. Alianzia Galilaya na sasa yupo hapa!”
Pilato Ampeleka Yesu Kwa Herode
6 Pilato aliposikia hili, akauliza, “Mtu huyu anatoka Galilaya?” 7 Akatambua kuwa Yesu yuko chini ya mamlaka ya Herode. Siku hizo Herode alikuwa Yerusalemu, hivyo Pilato alimpeleka Yesu kwake.
8 Herode alipomwona Yesu alifurahi sana. Alikuwa akisikia habari zake na kwa muda mrefu alikuwa anataka kukutana na Yesu. Herode alitaka kuona muujiza, hivyo alitegemea kwamba Yesu angefanya muujiza mmoja. 9 Akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini Yesu hakusema chochote. 10 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wamesimama pale wakipaza sauti zao wakimshitaki kwa Herode. 11 Ndipo Herode na askari wake wakamcheka. Wakamfanyia mzaha kwa kumvalisha mavazi kama ambayo wafalme huvaa. Kisha Herode akamrudisha Yesu kwa Pilato. 12 Nyakati za nyuma Pilato na Herode walikuwa maadui daima. Kuanzia siku ile wakawa marafiki.
Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu
(Mt 27:15-26; Mk 15:6-15; Yh 18:39-19:16)
13 Pilato aliwaita viongozi wa makuhani, viongozi wa Kiyahudi na watu wote pamoja. 14 Akawaambia, “Mlimleta mtu huyu kwangu. Mlisema alikuwa anawapotosha watu. Lakini nimemchunguza mbele yenu nyote na sijaona hatia juu ya kitu chochote mnachomshitakia. 15 Hata Herode hakumwona kuwa ana hatia yo yote. Akamrudisha kwetu. Tazameni, hajafanya jambo lolote baya linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo, baada ya kumwadhibu kidogo nitamwacha aende zake.” 17 [e]
18 Lakini wote walipaza sauti zao pamoja, “Mwue! Mwachie huru Baraba!” 19 (Baraba alifungwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo mjini na kwa mauaji.)
20 Pilato alitaka amwachie huru Yesu. Hivyo Pilato akawaambia atamwachilia. 21 Lakini walipaza sauti tena wakisema, “Mwue, Mwue msalabani!”
22 Mara ya tatu Pilato akawaambia watu, “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Hana hatia. Sioni sababu ya kumwua. Hivyo nitamwachia huru baada ya kumwadhibu kidogo.”
23 Lakini watu waliendelea kupaza sauti. Walidai Yesu auawe msalabani. Kelele zao zikawa kubwa kiasi kwamba 24 Pilato aliamua kuwapa kile walichotaka. 25 Walitaka Baraba aliyekuwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo na mauaji aachiwe huru. Pilato akamwachia Baraba. Na kumtoa Yesu ili auawe. Hili ndilo watu walitaka.
Yesu Awambwa Msalabani
(Mt 27:32-44; Mk 15:21-32; Yh 19:17-27)
26 Askari wakamwongoza Yesu kumtoa nje ya mji. Wakati huo huo mtu mmoja kutoka Kirene alikuwa anaingia mjini kutoka maeneo nje ya Yerusalemu. Askari wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu na kumfuata Yesu kwa nyuma.
27 Kundi kubwa wakamfuata Yesu. Baadhi ya wanawake waliokuwemo kwenye kundi walilia na kuomboleza. Walimwonea huruma. 28 Lakini Yesu aligeuka na kuwaambia, “Wanawake wa Yerusalemu, msinililie. Jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Wakati unakuja ambapo watu watasema, ‘Wanawake wasioweza kuwa na watoto ndio ambao Mungu amewabariki. Hakika ni baraka kwamba hawana watoto wa kutunza.’ 30 Watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni!’ Wataviambia vilima, ‘Tufunikeni!’(B) 31 Kama hili linaweza kutokea kwa mtu aliye mwema, nini kitatokea kwa wenye hatia?”
32 Walikuwepo pia wahalifu wawili waliotolewa nje ya mji pamoja na Yesu ili wauawe. 33 Walipelekwa mahali palipoitwa “Fuvu la Kichwa.” Askari walimpigilia Yesu msalabani pale. Waliwapigilia misalabani wahalifu pia, mmoja aliwekwa upande wa kulia na mwingine kushoto kwa Yesu.
34 Na Yesu alikuwa anasema, “Baba uwasamehe watu hawa, kwa sababu hawajui wanalofanya.”
Askari waligawana nguo zake kwa kutumia kamari. 35 Watu walisimama pale wakiangalia kila kitu kilichokuwa kinatokea. Viongozi wa Kiyahudi walimcheka Yesu. Walisema, “Kama kweli yeye ni Masihi, Mfalme Mteule wa Mungu, basi ajiokoe. Je, hakuwaokoa wengine?”
36 Hata askari walimcheka Yesu na kumfanyia mizaha. Walikuja na kumpa siki ya mvinyo. 37 Wakasema, “Ikiwa wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe!” 38 Waliandika maneno haya kwenye kibao msalabani juu ya kichwa chake: “Huyu ni Mfalme wa Wayahudi”.
39 Mmoja wa wahalifu aliyekuwa ananing'inia pale akaanza kumtukana Yesu: “Wewe siye Masihi? Basi jiokoe na utuokoe sisi pia!”
40 Lakini mhalifu mwingine alimnyamazisha asiendelee kumtukana Yesu. Akasema, “Unapaswa kumwogopa Mungu. Sisi sote tutakufa muda si mrefu. 41 Wewe na mimi tuna hatia, tunastahili kufa kwa sababu tulitenda mabaya. Lakini mtu huyu hajafanya chochote kibaya.” 42 Kisha akamwambia Yesu, “Unikumbuke utakapoanza kutawala kama mfalme!”
43 Yesu akamwambia, “Ninakwambia kwa uhakika, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.”
Yesu Afariki
(Mt 27:45-56; Mk 15:33-41; Yh 19:28-30)
44 Ilikuwa yapata saa sita mchana, lakini kulibadilika kukawa giza mpaka saa tisa alasiri, 45 kwa sababu jua liliacha kung'aa. Pazia ndani ya Hekalu lilichanika vipande viwili. 46 Yesu alipaza sauti akasema, “Baba, ninaiweka roho yangu mikononi mwako!”(C) Baada ya Yesu kusema haya, akafa.
47 Mkuu wa askari wa Kirumi aliyekuwa pale alipoona yaliyotokea, alimsifu Mungu, akisema, “Ninajua mtu huyu alikuwa mtu mwema!”
48 Watu wengi walikuwa wametoka mjini kuja kuona tukio hili. Walipoona, wakahuzunika, wakaondoka wakiwa wanapiga vifua vyao. 49 Watu waliokuwa marafiki wa karibu wa Yesu walikuwepo pale. Pia, walikuwepo baadhi ya wanawake waliomfuata Yesu kutoka Galilaya. Walisimama mbali kutoka msalabani, waliyaona mambo haya.
Yesu Azikwa
(Mt 27:57-61; Mk 15:42-47; Yh 19:38-42)
50-51 Mtu mmoja aliyeitwa Yusufu kutoka mji wa Uyahudi ulioitwa Arimathaya alikuwapo pale. Alikuwa mtu mwema, aliyeishi namna Mungu alivyotaka. Alikuwa anausubiri ufalme wa Mungu uje. Yusufu alikuwa mjumbe wa baraza la Kiyahudi. Lakini hakukubali pale viongozi wengine wa Kiyahudi walipoamua kumwua Yesu. 52 Alikwenda kwa Pilato na kumwomba mwili wa Yesu. 53 Aliushusha mwili kutoka msalabani na kuufunga kwenye nguo. Kisha akauweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika ukuta wa mwamba. Kaburi hili lilikuwa halijatumika bado. 54 Ilikuwa jioni Siku ya Maandalizi ya Sabato. Sabato ilikuwa ianze baada ya jua kuzama.
55 Wanawake waliotoka Galilaya pamoja na Yesu walimfuata Yusufu. Wakaliona kaburi. Ndani yake wakaona mahali alipouweka mwili wa Yesu. 56 Kisha wakaenda kuandaa manukato yanayonukia vizuri ili kuupaka mwili wa Yesu.
Siku ya Sabato walipumzika, kama ilivyoamriwa katika Sheria ya Musa.
Gavana Pilato Amhoji Yesu
(Mt 27:1-2,11-14; Mk 15:1-5; Yh 18:28-38)
23 Kisha kundi lote likasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2 Wakaanza kumshitaki Yesu na kumwambia Pilato, “Tumemkamata mtu huyu akijaribu kuwapotosha watu wetu. Anasema tusilipe kodi kwa Kaisari. Anajiita Masihi, mfalme.”
3 Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?”
Yesu akajibu, “Ndiyo, unaweza kusema hivyo.”
4 Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na watu, “Sioni kosa lolote kwa mtu huyu.”
5 Lakini waliendelea kusema, “Mafundisho yake yanasababisha matatizo katika Uyahudi yote. Alianzia Galilaya na sasa yupo hapa!”
Pilato Ampeleka Yesu Kwa Herode
6 Pilato aliposikia hili, akauliza, “Mtu huyu anatoka Galilaya?” 7 Akatambua kuwa Yesu yuko chini ya mamlaka ya Herode. Siku hizo Herode alikuwa Yerusalemu, hivyo Pilato alimpeleka Yesu kwake.
8 Herode alipomwona Yesu alifurahi sana. Alikuwa akisikia habari zake na kwa muda mrefu alikuwa anataka kukutana na Yesu. Herode alitaka kuona muujiza, hivyo alitegemea kwamba Yesu angefanya muujiza mmoja. 9 Akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini Yesu hakusema chochote. 10 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wamesimama pale wakipaza sauti zao wakimshitaki kwa Herode. 11 Ndipo Herode na askari wake wakamcheka. Wakamfanyia mzaha kwa kumvalisha mavazi kama ambayo wafalme huvaa. Kisha Herode akamrudisha Yesu kwa Pilato. 12 Nyakati za nyuma Pilato na Herode walikuwa maadui daima. Kuanzia siku ile wakawa marafiki.
Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu
(Mt 27:15-26; Mk 15:6-15; Yh 18:39-19:16)
13 Pilato aliwaita viongozi wa makuhani, viongozi wa Kiyahudi na watu wote pamoja. 14 Akawaambia, “Mlimleta mtu huyu kwangu. Mlisema alikuwa anawapotosha watu. Lakini nimemchunguza mbele yenu nyote na sijaona hatia juu ya kitu chochote mnachomshitakia. 15 Hata Herode hakumwona kuwa ana hatia yo yote. Akamrudisha kwetu. Tazameni, hajafanya jambo lolote baya linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo, baada ya kumwadhibu kidogo nitamwacha aende zake.” 17 [a]
18 Lakini wote walipaza sauti zao pamoja, “Mwue! Mwachie huru Baraba!” 19 (Baraba alifungwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo mjini na kwa mauaji.)
20 Pilato alitaka amwachie huru Yesu. Hivyo Pilato akawaambia atamwachilia. 21 Lakini walipaza sauti tena wakisema, “Mwue, Mwue msalabani!”
22 Mara ya tatu Pilato akawaambia watu, “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Hana hatia. Sioni sababu ya kumwua. Hivyo nitamwachia huru baada ya kumwadhibu kidogo.”
23 Lakini watu waliendelea kupaza sauti. Walidai Yesu auawe msalabani. Kelele zao zikawa kubwa kiasi kwamba 24 Pilato aliamua kuwapa kile walichotaka. 25 Walitaka Baraba aliyekuwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo na mauaji aachiwe huru. Pilato akamwachia Baraba. Na kumtoa Yesu ili auawe. Hili ndilo watu walitaka.
Yesu Awambwa Msalabani
(Mt 27:32-44; Mk 15:21-32; Yh 19:17-27)
26 Askari wakamwongoza Yesu kumtoa nje ya mji. Wakati huo huo mtu mmoja kutoka Kirene alikuwa anaingia mjini kutoka maeneo nje ya Yerusalemu. Askari wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu na kumfuata Yesu kwa nyuma.
27 Kundi kubwa wakamfuata Yesu. Baadhi ya wanawake waliokuwemo kwenye kundi walilia na kuomboleza. Walimwonea huruma. 28 Lakini Yesu aligeuka na kuwaambia, “Wanawake wa Yerusalemu, msinililie. Jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Wakati unakuja ambapo watu watasema, ‘Wanawake wasioweza kuwa na watoto ndio ambao Mungu amewabariki. Hakika ni baraka kwamba hawana watoto wa kutunza.’ 30 Watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni!’ Wataviambia vilima, ‘Tufunikeni!’(A) 31 Kama hili linaweza kutokea kwa mtu aliye mwema, nini kitatokea kwa wenye hatia?”
32 Walikuwepo pia wahalifu wawili waliotolewa nje ya mji pamoja na Yesu ili wauawe. 33 Walipelekwa mahali palipoitwa “Fuvu la Kichwa.” Askari walimpigilia Yesu msalabani pale. Waliwapigilia misalabani wahalifu pia, mmoja aliwekwa upande wa kulia na mwingine kushoto kwa Yesu.
34 Na Yesu alikuwa anasema, “Baba uwasamehe watu hawa, kwa sababu hawajui wanalofanya.”
Askari waligawana nguo zake kwa kutumia kamari. 35 Watu walisimama pale wakiangalia kila kitu kilichokuwa kinatokea. Viongozi wa Kiyahudi walimcheka Yesu. Walisema, “Kama kweli yeye ni Masihi, Mfalme Mteule wa Mungu, basi ajiokoe. Je, hakuwaokoa wengine?”
36 Hata askari walimcheka Yesu na kumfanyia mizaha. Walikuja na kumpa siki ya mvinyo. 37 Wakasema, “Ikiwa wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe!” 38 Waliandika maneno haya kwenye kibao msalabani juu ya kichwa chake: “Huyu ni Mfalme wa Wayahudi”.
39 Mmoja wa wahalifu aliyekuwa ananing'inia pale akaanza kumtukana Yesu: “Wewe siye Masihi? Basi jiokoe na utuokoe sisi pia!”
40 Lakini mhalifu mwingine alimnyamazisha asiendelee kumtukana Yesu. Akasema, “Unapaswa kumwogopa Mungu. Sisi sote tutakufa muda si mrefu. 41 Wewe na mimi tuna hatia, tunastahili kufa kwa sababu tulitenda mabaya. Lakini mtu huyu hajafanya chochote kibaya.” 42 Kisha akamwambia Yesu, “Unikumbuke utakapoanza kutawala kama mfalme!”
43 Yesu akamwambia, “Ninakwambia kwa uhakika, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.”
Yesu Afariki
(Mt 27:45-56; Mk 15:33-41; Yh 19:28-30)
44 Ilikuwa yapata saa sita mchana, lakini kulibadilika kukawa giza mpaka saa tisa alasiri, 45 kwa sababu jua liliacha kung'aa. Pazia ndani ya Hekalu lilichanika vipande viwili. 46 Yesu alipaza sauti akasema, “Baba, ninaiweka roho yangu mikononi mwako!”(B) Baada ya Yesu kusema haya, akafa.
47 Mkuu wa askari wa Kirumi aliyekuwa pale alipoona yaliyotokea, alimsifu Mungu, akisema, “Ninajua mtu huyu alikuwa mtu mwema!”
48 Watu wengi walikuwa wametoka mjini kuja kuona tukio hili. Walipoona, wakahuzunika, wakaondoka wakiwa wanapiga vifua vyao. 49 Watu waliokuwa marafiki wa karibu wa Yesu walikuwepo pale. Pia, walikuwepo baadhi ya wanawake waliomfuata Yesu kutoka Galilaya. Walisimama mbali kutoka msalabani, waliyaona mambo haya.
© 2017 Bible League International