Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Revised Common Lectionary (Complementary)

Daily Bible readings that follow the church liturgical year, with thematically matched Old and New Testament readings.
Duration: 1245 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Isa for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Waefeso 3:1-12

Huduma ya Paulo kwa Wasio Wayahudi

Hivyo, mimi Paulo ni mfungwa kwa sababu ninamtumikia Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi msio Wayahudi. Mnajua hakika ya kuwa Mungu alinipa kazi hii kupitia neema yake ili niwasaidie. Mungu alinionyesha na nikaweza kuujua mpango wake wa siri. Nimekwisha kuandika kiasi fulani juu ya hili. Na ikiwa mtasoma nilichowaandikia, mtajua kuwa ninaielewa siri ya kweli kuhusu Kristo. Watu walioishi zamani hawakuambiwa siri hiyo. Lakini sasa, kupitia Roho, Mungu amewawezesha mitume na manabii wake watakatifu kuijua siri hiyo. Na siri hiyo ni hii: Kwa kuikubali Habari Njema, wale wasio Wayahudi watashiriki pamoja na Wayahudi katika baraka alizonazo Mungu kwa ajili ya watu wake. Wao ni sehemu ya mwili mmoja, na wanashiriki manufaa ya ahadi ambayo Mungu aliitimiza kupitia Kristo Yesu.

Kwa kipawa cha neema ya Mungu, nilifanywa mtumishi wa kuihubiri Habari Njema. Alinipa neema hiyo kwa nguvu zake. Mimi nisiye na umuhimu zaidi miongoni mwa watu wa Mungu. Lakini alinipa kipawa hiki cha kuwahubiri wasio Wayahudi Habari Njema kuhusu utajiri alionao Kristo. Utajiri huu ni mkuu na si rahisi kuuelewa kikamilifu. Pia Mungu alinipa kazi ya kuwaambia watu kuhusu mpango wa siri yake ya kweli. Aliificha siri hii ya kweli ndani yake tangu mwanzo wa nyakati. Ndiye aliyeumba kila kitu. 10 Lengo lake lilikuwa kwamba watawala wote na mamlaka zote zilizo mbinguni zijue njia nyingi anazotumia kuionesha hekima yake. Watalijua hili kwa sababu ya kanisa. 11 Hii inaendana na mpango aliokuwa nao Mungu tangu mwanzo wa nyakati. Alitekeleza mpango wake kupitia Kristo Yesu Bwana wetu. 12 Kwa kuwa tu wake Kristo tunakuja mbele za Mungu tukiwa huru bila woga. Tunaweza kufanya hivi kwa sababu ya uaminifu wake Kristo.[a]

Mathayo 2:1-12

Wenye Hekima Waja Kumwona Yesu

Yesu alizaliwa katika mji wa Bethlehemu ya Uyahudi wakati Herode alipokuwa mfalme. Baada ya Yesu kuzaliwa, baadhi ya wenye hekima kutoka mashariki walikuja Yerusalemu. Walipofika wakawauliza watu, “Yuko wapi mtoto aliyezaliwa ili awe Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota ilipochomoza na kutuonesha kuwa amezaliwa. Nasi tumekuja ili tumwabudu.”

Mfalme Herode aliposikia haya, yeye pamoja na watu wote wakaao Yerusalemu walikasirika sana. Herode aliitisha mkutano wa wakuu wote wa makuhani wa Kiyahudi na walimu wa sheria. Akawauliza ni wapi ambapo Masihi angezaliwa. Wakamjibu, “Ni katika mji wa Bethlehemu ya Yuda kama ambavyo nabii aliandika:

‘Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
    wewe ni wa muhimu miongoni mwa watawala wa Yuda.
Ndiyo, mtawala atakayewaongoza
    watu wangu Israeli, atatoka kwako.’”(A)

Kisha Herode akawaita na kufanya mkutano wa siri na wenye hekima kutoka mashariki. Akaelewa kwa usahihi wakati walipoiona nyota. Kisha akawaruhusu waende Bethlehemu. Akawaambia, “Nendeni mkamtafute mtoto kwa makini na mtakapompata mrudi na kunipa taarifa mahali alipo, ili nami pia niende kumwabudu.”

Wenye hekima walipomsikiliza mfalme, waliondoka. Waliiona tena ile nyota waliyoiona hapo mwanzo na wakaifuata. Nyota ile iliwaongoza mpaka mahali alipokuwa mtoto na kusimama juu ya sehemu hiyo. 10 Wenye hekima walipoona kuwa nyota ile imesimama, walifurahi na kushangilia kwa furaha.

11 Wenye hekima hao kisha waliingia katika nyumba alimokuwamo mtoto Yesu pamoja na Mariamu mama yake. Walisujudu na kumwabudu mtoto. Kisha wakafungua masanduku yenye zawadi walizomletea mtoto. Wakampa hazina za dhahabu, uvumba na manemane. 12 Lakini Mungu aliwaonya wenye hekima hao katika ndoto kuwa wasirudi tena kwa Herode. Hivyo kwa kutii walirudi nchini kwao kwa kupitia njia nyingine.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International